DR REMMY ONGALA: Kwa Nini Alitaka Kufukuzwa Tanzania? | Siri ya “Dr. Remmy” na Safari Yake ya Mwisho
IKUMBUKWE
0:00 / 0:00
DR REMMY ONGALA: Kwa Nini Alitaka Kufukuzwa Tanzania? | Siri ya “Dr. Remmy” na Safari Yake ya Mwisho
37 570 просмотров · 2 мес. назад
IKUMBUKWE
28 тыс. подписчиков
37 570 просмотров · 2 мес. назад
e, unajua kwamba Remmy Ongala aliwahi kutishiwa kufukuzwa Tanzania? Kwa nini hakuwahi kurudi Congo tangu alipofika Dar es Salaam mwaka 1978? Na kwa nini dunia ilimfahamu kama “Dr. Remmy” wakati hakuwa daktari wa tiba?
Katika episode hii maalum ya IKUMBUKWE, tunafungua kurasa ambazo wengi hawajawahi kuzisikia kuhusu maisha ya Ramazani Mtoro “Remmy” Ongala.
Kupitia mahojiano ya kipekee na:
Aziza Ongala – binti yake, akieleza Remmy kama baba na namna familia inavyohifadhi urithi wake.
Tom Ongala – mwanawe na mrithi wa muziki wa Super Matimila, akisimulia safari ya muziki na dakika za mwisho za maisha ya baba yake.
Masoud Masoud – mtangazaji mkongwe, akichambua uandishi wa nyimbo za Remmy, ushawishi wake kwa jamii na mazingira yaliyopelekea kutishiwa kufukuzwa nchini.
Hii si simulizi ya muziki pekee, bali ni historia ya mtu aliyekuwa sauti ya mnyonge, aliyethubutu kuimba kuhusu umaskini, rushwa, UKIMWI na maisha ya mwananchi wa kawaida. Nyimbo zake ziliwahi kuzua mijadala, lakini pia zilimjengea heshima kubwa ndani na nje ya Tanzania.
Subscribe kwa IKUMBUKWE kwa simulizi zaidi za historia, muziki na watu walioacha alama Tanzania na Afrika.