Перейти к содержимому

MAKAMU WA RAIS ATOA MAAGIZO HAYA EL - NINO "ONDOENI UCHAFU MARA MOJA"

Daily News Digital

0:00 / 0:00

MAKAMU WA RAIS ATOA MAAGIZO HAYA EL - NINO "ONDOENI UCHAFU MARA MOJA"

4 530 просмотров · 22 часа назад
Daily News Digital
284 тыс. подписчиков
4 530 просмотров · 22 часа назад
DAR ES SALAAM: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameagiza Mamlaka na Taasisi zinazohusika kuchukua hatua za haraka kujiandaa ili kuzuia na kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño zinazotarajiwa kuanza mwezi Oktoba 2026. Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo, mara baada ya kupokea taarifa ya utayari na maandalizi ya Serikali kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuhusu mvua za El- nino, katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Viongozi pamoja na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Wizara ya Ujenzi pamoja na Taasisi zilizochini ya Wizara hizo, Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa taasisi zote zinazohusika, kufanya kazi kwa pamoja na kuchukua hatua za tahadhari mapema ili kuzuia au kupunguza athari zinazoweza kutokea kwa wananchi kufuatia ujio wa mvua hizo. Follow us on: FACEBOOK; SpotiLeo:   / spotileo-176.  . HabariLeo:   / habarileo   DailyNews:   / dailynewstz   INSTAGRAM; HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig... SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid... TWITTER; Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09