Перейти к содержимому

🔴 MASISI : WAZALENDO NA MAKOLONELI WAMEJIUNGA NA AFC-M23 HUKO KASENYI

KIVU MORNING POST

0:00 / 0:00

🔴 MASISI : WAZALENDO NA MAKOLONELI WAMEJIUNGA NA AFC-M23 HUKO KASENYI

3 573 просмотра · 1 день назад
KIVU MORNING POST
374 тыс. подписчиков
3 573 просмотра · 1 день назад
Katika mashariki mwa DRC, wapiganaji 22 wa Wazalendo wa kundi la PARECO la Jeneral Mutayomba, wakiwemo makolonele wawili, walijisalimisha kwa AFC-M23 Jumatano tarehe 2 Septemba huko Kasenyi, katika wilaya ya Masisi. Msimamizi wa wilaya ya Masisi, Emmanuel Ndizeye Rutebuka, aliwapokea. Kati ya wapiganaji hao 22 kuna wasichana na wavulana watatu walio chini ya miaka 18. Waliojisalimu wameeleza sababu zilizowafanya kujisalimisha kwa AFC-M23. Kwa Emmanuel Ndizeye Rutebuka, kujisalimisha kwao ni jambo la kuridhisha. Mapigano makali kwa kutumia silaha nzito yanaendelea tangu saa saba mchana Alhamisi tarehe 3 Septemba 2026, kati ya wapiganaji wa AFC-M23 na muungano wa Wazalendo-FARDC huko Chinono, kwenye mpaka wa maeneo ya Ziralo na Mubuku, katika chefferie ya Buhavu, wilaya ya Kalehe, Kusini-Kivu, mashariki mwa DRC. Kwa mujibu wa jamii ya kiraia ya eneo hilo, mapigano hayo yamesababisha wakazi wengi kukimbia makazi yao. Baadhi yao wanaelekea Ramba, katika eneo la Mubuku, wakati wengine wamekimbilia porini. Kusini-Kivu, shirika la Association Debout Kamituga linaomba msaada wa wananchi ili kukarabati Hospitali Kuu ya Kamituga, katika wilaya ya Mwenga, Kusini-Kivu. Dhoruba kali iliyotokea Juni 2026 iling’oa paa la wodi ya wazazi na kusababisha uharibifu mkubwa unaokadiriwa kuwa dola 51,000 za Marekani. Shirika hilo linaonya kuhusu umuhimu wa kukarabati haraka hospitali hiyo, ambayo ni muhimu katika kuwahudumia kina mama na watoto wachanga 📢 À propos de KivuMorningPost KivuMorningPost est la source numéro un d'information en RDC Congo, spécialisée dans la couverture de l'actualité de l'Est du pays depuis Goma, au Nord-Kivu. Notre mission est claire : informer pour transformer. Nous publions des contenus fiables, exclusifs et locaux sur la politique, les conflits, l'économie, la société et la culture congolaise. 📍 Basé à Goma – Nord-Kivu | RDC Congo 🔎 Recherchez “KivuMorningPost” sur Google, YouTube, ou TikTok pour rester informé sur l’actualité en RDC. 🌐 Restez connectés avec nous : 📧 Email : kivumorningpost@gmail.com 🌍 Site Web : www.kivumorningpost.com 📺 YouTube : Chaîne KivuMorningPost 👍 Facebook : KivuMorningPost 🐦 Twitter (X) : @KivuMorningPost 📸 Instagram : @kivumorningpostofficial 🎵 TikTok : @kivumorningpost