Перейти к содержимому

SOTE TUJENGE NCHI YETU KWA KUCHANGIA MAPATO – MWENYEKITI WA AMCOS MKOA WA MANYARA

TRA ONLINE TV

0:00 / 0:00

SOTE TUJENGE NCHI YETU KWA KUCHANGIA MAPATO – MWENYEKITI WA AMCOS MKOA WA MANYARA

33 просмотра · 2 дня назад
TRA ONLINE TV
17,6 тыс. подписчиков
33 просмотра · 2 дня назад
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Manyara leo, Septemba 17, 2026, kupitia mpango wake wa "_Alhamisi ya Kusikiliza Walipakodi_", imemtembelea na kufanya mahojiano maalum na Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS) Mkoa wa Manyara, Bw. Omari Mazinde, lengo likiwa ni kuisikia sekta ya kilimo na kuimarisha ushirikiano katika usimamizi wa kodi. Katika mahojiano hayo ya video, Bw. Omari Mazinde ametoa shukrani za dhati kutoka kwa wakulima wa miwa mkoani hapo kwenda kwa Serikali na TRA kwa maridhiano mazuri na rafiki yaliyofikiwa na kufanikisha uuzaji wa zao la miwa, huku mamlaka hiyo ikiwawezesha kutoa risiti za kielektroniki (EFD) kwa urahisi kupitia mfumo mpya wa IDRAS. Akimalizia ujumbe wake, Bw. Mazinde ametoa wito kwa wananchi, wakulima, na wafanyabiashara wote mkoani Manyara kujitokeza na kulipa kodi stahiki kwa hiari na kwa wakati, akisisitiza kuwa "sote tujenge nchi yetu kwa kuchangia mapato" ili kuiletea nchi maendeleo endelevu.