BODABODA WAONYWA KUENDESHA YOMBO VYA MOTO BILA YA LESENI
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
BODABODA WAONYWA KUENDESHA YOMBO VYA MOTO BILA YA LESENI
1 122 просмотра · 4 дн. назад
ASAM Online TV
22,7 тыс. подписчиков
1 122 просмотра · 4 дн. назад
Viongozi wa Jimbo la Amani, Mkoa wa Mjini Magharibi, wamefanya ziara ya kutembelea vikundi mbalimbali vya waendesha bodaboda, gereji na wajasiriamali kwa lengo la kuhamasisha ushirikiano na kuwahimiza kujisajili katika vikundi vyao.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mbunge wa Jimbo la Amani, Mhe. Abdul Yussuf Maalim, amesema ziara hiyo ni sehemu ya utaratibu mpya wa kuwafikia wananchi na makundi mbalimbali ya kijamii ili kuwafahamisha fursa za maendeleo, ikiwemo kupata misaada kutoka serikalini na huduma za kifedha kupitia benki.
Ameeleza kuwa vikundi vilivyosajiliwa vina nafasi nzuri ya kusaidiana vinapokabiliwa na changamoto mbalimbali, sambamba na kunufaika na fursa zinazopatikana kupitia mifumo rasmi ya vikundi.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Jimbo la Amani, Mhe. Masoud Amour Masoud, amewahimiza vijana wanaojihusisha na usafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki maarufu kama bodaboda kuhakikisha wanamiliki leseni halali za udereva ili kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Amesisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha vijana hao wanafanya kazi katika mazingira salama na yanayozingatia sheria.
#AsamOnlineTV #Zanzibar #Amani #Bodaboda #Wajasiriamali