KAMATI YA MAENDELEO WDC YATINGA KILOLE, YATOA MAELEKEZO
AMASHI TV
0:00 / 0:00
KAMATI YA MAENDELEO WDC YATINGA KILOLE, YATOA MAELEKEZO
165 просмотров · 12 дней назад
AMASHI TV
7,18 тыс. подписчиков
165 просмотров · 12 дней назад
Kukamilika kwa miradi ya maendeleo kunatajwa kuwa chachu ya kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi, kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za serikali.
Katika Kata ya Kilole, jitihada hizo zinaendelea kushika kasi, huku Kamati ya Maendeleo ya Kata chini ya diwani wake ali mkwavingwa ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji korogwe ikifanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kilole, Ofisi ya Mtaa wa Kambi ya Maziwa na ukarabati wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Kwamngumi.
Ziara inaanza katika eneo la ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kilole, mradi unaotarajiwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma kwa wananchi pamoja na kurahisisha upatikanaji wa wataalam na huduma mbalimbali za serikali kama anavyoeleza Mtendaji wa Kata ya Kilole, Janeth Richard Mbutu.
Kutoka Ofisi ya Kata, ziara inaelekea Mtaa wa Kambi ya Maziwa, ambako ujenzi wa ofisi ya mtaa unaendelea.
Baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi, Diwani wa Kata ya Kilole, Ali Mkwavingwa, ametoa maelekezo ya kuhakikisha hatua ya ujenzi iliyoanza inakamilishwa ili wananchi waanze kunufaika na huduma katika ofisi hiyo.
Kutoka kwenye miradi ya ofisi za serikali, safari ya ziara inaingia katika sekta ya elimu.
Katika Shule ya Msingi Kwamngumi, Diwani wa Kata ya Kilole, Ali Mkwavingwa, anatumia nafasi hiyo kuzungumza na wanafunzi wa Darasa la Saba na anawatia moyo kuelekea mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi