Перейти к содержимому

MAOMBI YA ASUBUHI ILI KUHARIBU ROHO YA MAPOOZA - S1EP4

Maombi Madhabahuni

0:00 / 0:00

MAOMBI YA ASUBUHI ILI KUHARIBU ROHO YA MAPOOZA - S1EP4

321 просмотр · Трансляция закончилась 1 г. назад
Maombi Madhabahuni
2,17 тыс. подписчиков
321 просмотр · Трансляция закончилась 1 г. назад
Kupitia MTIRIRIKO WA MAOMBI HAYA YA ASUBUHI; Mtumishi wa BWANA atakufundisha na kukusaidia katika mambo yafuatayo: TUNANG’OA JE ROHO ZA MAPOOZA? UKWELI KUHUSU KUZAA MAPOOZA KATIKA BIBLIA KUNG'OA ROHO ZA KUZAA MAPOOZA Kuzaa mapooza maana yake ni kuzaa kitu kilichokufa , au inalinganishwa na kuzaa kitu ambacho hakina uhai,au kwa maana nyingine ni kutokuzaa kabisa, au kwa maana nyingine ni kupukutisha matunda maana yake kuzaa kitu ambacho hakijakomaa. Unaweza ukaanzisha vitu vyako vizuri kabla havijakomaa vinakufa ,kwahiyo maana nyingine ya kuzaa mapooza ni kufa kabla ya wakati. Hii maana yake ni kuzaa mapooza. Imeandikwa katika MALAKI 3:11 “Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.Kwahiyo kupukutisha majani kabla ya wakati” Katika kitabu cha 2 WAFALME 2:19 "Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza." Ukiisoma aya hii vizuri utagundua kuwa ni kweli mji huu ulikuwa mzuri kw akila hali. Ni kama ambavyo hata leo hii mji wetu wa Morogoro watu wanausifia kuwa ni mzuri, wakiupa Jina la “Mji kasoro bahari”. Lakini pamoja na uzuri wote huu, mji huu huu watu wanachukuliwa msukule. Mji unazaa mapooza: Watu hawajengi nyumba zao, na wakijenga ujenzi haumaliziki; Watu wa mji ule walipouangalia mji wakagundua mji ule ni mzuri lakini huzaa mapooza. Elisha alipoona mji ule una matatizo kwanza aliwauliza shida hii imeanzia wapi ,ni vizuri kujua chanzo cha tatizo ukishakijua chanzo cha tatizo ukakishughulikia utakua umemaliza tatizo, Elisha akaagiza aletewe chumvi akaagiza apelekwe kwenye ile chemchemi ya maji akatamka neno juu ya yale maji, ni vizuri kila unapokuja kanisani utamkiwe neno juu ya maisha yako,ni kweli wamepanda mapooza kwenye ndoa yako, kwenye kazi yako,elimu yako lakini leo Bwana anakwenda kuweka chumvi kwenye chanzo cha tatizo lako na chumvi hiyo ni neno la kristo,neno la kristo ni uhai likaondoe mapooza kwenye shida yako,kile unachokiamini ndicho utakachokipokea ,wana wa Israeli walipofika jangwani wakaanza kumlalamikia musa na kumwambia ni bora ungetuacha misri kuliko kutuleta mahali hapa, lakini Biblia inatuambia walifia wote jangwani walibaki watu wawili tu, ushindi wako unategemea unatamka nini ,jifunze kutamka maneno ya ushindi hata kama unaona hamna kitu kinachoendelea wewe tamka maneno ya ushindi, Ni kweli yamepandwa mapooza, jamii, kazi, familia, katika maisha yako, lakini mimi leo nakuja kwako kama neno la Kristo. Usihangaike na chumvi zinazotolewa na wahubiri mbalimbali nyakati hizi. Wengi wao wanawaza kwa kuwa Elisha alitumia chumvi basin a wao wautumie ufunuo huo huo. Ni kawaida endapo mtu utanyweshwa chumvi nyingi kutapika lazima utatapika. Cha kufanya siyo kutumia chumvi bali neno la Kristo kaw kuwa neno la Kristo ni kila kitu maishani mwetu. Kazi yangu ni nzuri lakini inazaa mapooza. Ndo yangu ni nzuri lakini inazaa mapooza. Leo tunayang’oa kila mapando ya mapooza kwa Jina la Yesu. Pengine una mume wako ulimpenda sana katika uchumba wako, lakini kwa kuwa hukufuata taratibu za kanisa ukaanza kuishi naye bila ndoa. Yamkini mume huyo huyo alikudanganya kuwa hata yeye anampenda Bwana Yesu ingawa siyo wa kanisani mwako. Leo hii maisha yako yamekuwa magumu na ajabu kwa sababu mume huyo ni mlevi na amekuwa akikuletea akina mama wengine ndani ya nyumba hiyo hiyo. Cha kufahamu hapo ni kuwa, ndoa yako ilikuwa nzuri lakini imezaa mapooza.