Перейти к содержимому

AJALI MBAYA MANDIWA, WATU WAPOTEZA MAISHA WENGINE WAJERUHIWA

MUUNGWANA ONE TV

0:00 / 0:00

AJALI MBAYA MANDIWA, WATU WAPOTEZA MAISHA WENGINE WAJERUHIWA

524 просмотра · 1 мес. назад
MUUNGWANA ONE TV
8,27 тыс. подписчиков
524 просмотра · 1 мес. назад
Leo ni Jumapili, tarehe 16 Agosti 2026. Muungwana One TV tupo katika eneo la Mandiwa, Kata ya Chigugu, Wilaya ya Masasi, Mkoa wa Mtwara, ambako kumetokea ajali mbaya ya gari la abiria lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Masasi. Ajali hiyo imetokea jana, tarehe 15 Agosti 2026, majira ya saa 2:00 usiku, katika Kijiji Cha Mandiwa, maeneo ya Darajani. Kwa mujibu wa taarifa za awali, gari hilo linadaiwa kuwa la kampuni ya Maning’inice, limegonga mtu aliyekuwa akiendesha baiskeli, ambaye inadaiwa amefariki papo hapo. Katika ajali hiyo, abiria kadhaa wamejeruhiwa, na baadhi yao wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Ndanda kwa ajili ya matibabu. Muungwana One TV tupo hapa eneo la tukio kufuatilia kwa karibu kilichotoke a, kuzungumza na mashuhuda pamoja na mamlaka husika, ili kuwafikishia taarifa sahihi kuhusu ajali hii, idadi ya waliofariki na hali ya majeruhi. Update Muungwana One tv