Перейти к содержимому

JULIO:IBRAHIM DOUMBIA MPIRA HAJUI KABISA,NAMZIDI HATA MIMI NA KITAMBI CHANGU SIMBA WAACHANE NAYE

MABENA TV

0:00 / 0:00

JULIO:IBRAHIM DOUMBIA MPIRA HAJUI KABISA,NAMZIDI HATA MIMI NA KITAMBI CHANGU SIMBA WAACHANE NAYE

847 просмотров · 17 часов назад
MABENA TV
114 тыс. подписчиков
847 просмотров · 17 часов назад
#julio #simbasc #ibrahimdoumbia #usajilimpyawasimba JULIO ASHINDWA KUJIZUIA KWA DOUMBIA, AMGUSA PIA MGUNDA Kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio' ameshindwa kujizuia na kumvaa Ibrahim Doumbia wa Simba akisema hajui mpira na anapaswa kutemwa na klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili. Pia Julio aliyewahi kutamba na klabu za CDA Dodoma, Pilsner na Simba enzi za uchezaji wake kabla ya kugeukia ukocha, pia alimchambua Ismail Mgunda akisema ni mchezaji asiyetaka kujisumbua licha ya kuwa straika mwenye kila kitu kwa sasa nchini. Akihojiwa na kipindi cha michezo za EFM Radio, Julio alisema hana cha kuficha wala kumtetea Doumbia kwa kushindwa kufanya maajabu tangu atue Msimbazi. Julio alisema Doumbia hajui mpira na anashangaa waliomsajili na kupinga wale wanaomtetea eti aendelee kupewa muda zaidi. "Mie simumunyi maneno, Doumbia hajui mpira na ifike wakati klabu zizingatie agizo la Rais wa TFF (Walace Karia), nyota wa kigeni wanaokuja nchi wawe wanazichezea timu za taifa na sio mizigo kama hawa, " amenukuliwa Julio akisisitiza kuna wachezaji wengi wa kigeni aina ya Doumbia wanaozidiwa viwango na wachezaji wazawa. Alipoulizwa kuhusu Ismail Mgunda aliuesajiliwa kutoka Mashujaa klabu aliyowahi kuinoa, amesema ni mchezaji mzuri lakini hapendi kujisumbua kujituma kitu alichowahi kuzungumza naye a alipokuwa naye Mashujaa na hata timu ya taifa. "Kama atanisikia na kuchukia sijali, ila ni kwamba huyu (Mgunda) ni mchezaji mzuri iwapo atajituma. Ana mwili mkubwa, nguvu na anajua soka, tatizo ni kama ameridhika na kukubali kuwa hivyo alivyo wakati yeye ni tegemeo hata kwa taifa," amesema Julio. Julio amesema hakubaliani na suala la kuwapa muda zaidi wachezaji wapya, akisema mchezaji anayejua soka na anayejitambua akipata nafasi tu hufanya mambo, akiwatolea mfano Albert Kangwanda wa Yanga, Anthony Mligo, Nickson kibabage, Nathaniel Chilambo na hata Libasse Gueye wanaotamba Simba baada ya kupewa nafasi. Doumbia amekuwa gumzo kwa kushindwa kufunga bao tangu aanze kuitumikia Simba na ishu ya kuwa presha kubwa klabuni, Julio alisema mchezaji mkubwa hasumbuliwi na vitu kama hivyo kama anajua soka na kusisitiza klabu zisipoteze pesa kwa kuleta wachezaji wasio na uwezo wala viwango bora. Unakubaliana na msimamo wa Julio kuwa Doumbia hajui soka?