Перейти к содержимому

RC Kilimanjaro Ahimiza Utalii wa Ndani, Awataka Wananchi Kutembelea Mkomazi

KILIMANJARO REVIVAL TV

0:00 / 0:00

RC Kilimanjaro Ahimiza Utalii wa Ndani, Awataka Wananchi Kutembelea Mkomazi

71 просмотр · 2 недели назад
KILIMANJARO REVIVAL TV
53 подписчика
71 просмотр · 2 недели назад
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amewataka wananchi kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, iliyopo kati ya mikoa ya Kilimanjaro na Tanga, huku akihamasisha kutangazwa kwa vivutio vya hifadhi hiyo. Ameyasema hayobaada ya kuandaa safari maalum ya waandishi wa habari wa mkoa huo kwenda Mkomazi, kwa lengo la kuwapa fursa ya kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo na kuvitangaza kwa wananchi. Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Eva Malya, amewakaribisha wananchi kutembelea hifadhi hiyo, akisema ina wanyamapori wa ‘Big Five’, ikiwemo Simba, Chui, Tembo, Mbogo na fursa ya utalii wa faru, huku akieleza kuwa gharama za kutembelea hifadhi hiyo ni nafuu sana.