Перейти к содержимому

Dondoo za Ufugaji na Daktari wa Zamu

Harvest Point limited

0:00 / 0:00

Dondoo za Ufugaji na Daktari wa Zamu

472 просмотра · 5 мес. назад
Harvest Point limited
260 подписчиков
472 просмотра · 5 мес. назад
Leo, katika mwendelezo wa kipindi chetu cha Dondoo za Ufugaji na Daktari wa Zamu, timu ya wataalamu kutoka Harvest Point Limited ilifanya ziara kwa mmoja wa wafugaji wetu aliyejiunga nasi hivi karibuni. Lengo kuu lilikuwa ni kuboresha mifumo ya ufugaji ili kuhakikisha mfugaji anapata matokeo bora na ya kitaalamu. Miongoni mwa mambo muhimu yaliyoshauriwa ni: Mfumo sahihi wa taa na umuhimu wa mwanga kwa uzalishaji wa kuku wa mayai Kutenga kuku wagonjwa badala ya kuwaacha ndani ya mfumo wa cage Umuhimu wa kuweka ventilation (vents) kwenye banda kwa mzunguko mzuri wa hewa Utunzaji sahihi wa dawa na uteketezaji salama wa mabaki yake Matumizi ya footbath mlangoni na kubadilisha dawa kila baada ya siku tatu Usimamizi bora wa taka (waste management) kwa kutupa mbolea mbali na banda Tunajivunia kuwa karibu na wafugaji wetu, tukitoa siyo tu chakula bora cha kuku, bali pia maarifa ya vitendo yanayoleta matokeo halisi shambani. Jiunge nasi kila Jumamosi ujifunze zaidi kupitia kipindi chetu cha Dondoo za Ufugaji na Daktari wa Zamu 📞 Tupigie: +255 746 482 566 #DondooZaUfugaji #DaktariWaZamu #chakulachakuku #HarvestPoint