Перейти к содержимому

EPISODE 92: LISSU AWAAMBIA MAJAJI MSIITIKIE WITO WA KUNINYONGA HADI KUFA KWA USHAHIDI WA HISIA

UHURU MEDIA ONLINE

0:00 / 0:00

EPISODE 92: LISSU AWAAMBIA MAJAJI MSIITIKIE WITO WA KUNINYONGA HADI KUFA KWA USHAHIDI WA HISIA

52 662 просмотра · 9 часов назад
UHURU MEDIA ONLINE
350 тыс. подписчиков
52 662 просмотра · 9 часов назад
EPISODE 92: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameiambia mahakama kwamba kesi ya uhaini dhidi yake imejengwa katika msingi wa hisia na haina ushahidi thabiti unaokubalika kisheria ili kuthibitisha kama kulikuwa na nia ya kutenda kosa la kihaini. Lissu amesema hayo leo Septemba 24, 2026, alipokuwa akiendelea kufanya uwasilishaji wa hoja za mwisho (final submission) mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, ambo wanasikiliza kesi hiyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam. "Walionishtaki wanataka kunihukumu kifo kwa sababu ya hisia zao, kwa sababu wanahisi nilikuwa nataka kuitishia Serikali." Amesema Lissu. Lissu ameongeza zaidi kwamba, upande wa mashtaka na mawakili wamerudia madai ya kosa la uhaini kwa kisingizio kuwa uchaguzi unafanywa kwa mujibu wa katiba na Serikali ndiyo inasimamia katiba, huku akihoji kama serikali ndiyo chombo pekee kinachosimamia katiba wakati zipo sheria zinazosimamiwa na mihimili mingine kama vile Mahakama na Bunge, na akihoji pia kama Tume ya Uchaguzi ni serikali. Aidha, amesema kuwa kujenga kesi nzito kama ya uhaini ambayo ni kosa pekee lililotajwa katika Katiba ya Tanzania kwa kutumia hisia tupu hakuwezi kuwa msingi halali wa kumtia mtu hatiani. "Hii si kesi ya mauaji ni kesi ya uhaini na ni kosa pekee ambalo limetajwa katika katiba ya Tanzania, na kuhisi tu huyu mtu anailenga serikali hata kama huyu mtu ana hisia hizo kiasi gani haziwezi kuwa msingi wa kumtia mtu hatiani." Ameongeza Lissu. Akieleza zaidi kuhusu misingi ya kisheria, amesisitiza kuwa mahakama haiwezi ikawakubalia upande wa mashtaka na akawaomba majaji kutoitikia wito wa mashtaka hayo ambayo amesema yamejengwa kwa hisia za walioshtaki badala ya ushahidi thabiti wa kisheria. #tundulissu #mahakamani