ASKOFU DKT.SHOO AZINDUA NYUMBA YA IBADA ILIYOJENGWA KWA ZAIDI YA BILIONI 2 USHARIKA WA MAJENGO
UMOJA DAIMA MEDIA
0:00 / 0:00
ASKOFU DKT.SHOO AZINDUA NYUMBA YA IBADA ILIYOJENGWA KWA ZAIDI YA BILIONI 2 USHARIKA WA MAJENGO
2 081 просмотр · 1 г. назад
UMOJA DAIMA MEDIA
3,58 тыс. подписчиков
2 081 просмотр · 1 г. назад
Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Askofu Dkt. Frederick Onael Shoo amezindua rasmi nyumba ya ibada Usharika wa Majengo leo tarehe 20/7/2025.
Akizindua nyumba hiyo ya ibada Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Dkt. Fredrick Shoo amepongeza kukamilika kwa Kanisa hilo lililojengwa kwa miaka 15.
Dkt. Shoo amewapongeza washarika wa Majengo kwa kushiriki kikamilifu kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo ya ibada yenye uwezo wa kupokea idadi ya washarika zaidi ya 1,200 kwa mara moja
"Niwapongeze mno kwa kazi hii kubwa ambapo kwa asilimia kubwa imefanywa na washarika wa Usharika huu pamoja na marafiki kutoka madhehebu mengine, ujenzi wa Makanisa pacha la Majengo na Njoro yamejengwa kwa nguvu zenu wenyewe bila msaada wa ufadhili kutoka nje, huu ni mfano mzuri kwa Makanisa mengine" alisema Dkt.Shoo