“HATA MSIBANI HAKUNIACHA!” VISU, VITISHO NA MATUSI VYAWAFIKISHA WANANCHI POLISI
TMC NEWS TV
0:00 / 0:00
“HATA MSIBANI HAKUNIACHA!” VISU, VITISHO NA MATUSI VYAWAFIKISHA WANANCHI POLISI
331 просмотр · 2 дн. назад
TMC NEWS TV
42,4 тыс. подписчиков
331 просмотр · 2 дн. назад
Wakazi wa Maili Mbili na Ostabei jijini Dodoma wameeleza kero za kiusalama wanazodai kukabiliana nazo katika maeneo yao, zikiwemo vitisho vya kuuawa, madai ya watu kutembea na visu, ukabaji, matusi ya nguoni na usumbufu unaohusishwa na baadhi ya vijana kunywa pombe hadi usiku.
Katika mkutano na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini, SSP Daud Nkuba, mkazi Fatuma Rashid Ally amedai kutishiwa maisha na kufuatwa hadi kwenye msiba. Wakazi wengine wameeleza hofu zao kuhusu vitisho na kelele za usiku, huku mkazi mwingine akiomba kufuatiliwa kwa kesi inayohusu madai ya kupigwa kwa baba yake mdogo.
Wananchi wameiomba polisi kufuatilia malalamiko hayo na kuchukua hatua stahiki ili kurejesha amani na usalama katika maeneo yao.
Je, SSP Daud Nkuba amejibu nini kuhusu kilio cha wananchi? Tazama ushuhuda wao na majibu ya polisi katika video hii.
NEWS | Shaping The Future
Asante kwa kufuatilia TMC NEWS. Subscribe, Like na Share ili kuendelea kupata habari za uhakika, matangazo ya moja kwa moja na uchambuzi wa kina kutoka Tanzania na duniani.
🔔 Washa arifa (Notifications) ili usipitwe na taarifa muhimu.
📢 Kwa matangazo, ushirikiano na maoni:
📧 tmcnewsmedia@gmail.com
📞 +255 674 075 414
🌐 Tufuatilie kwenye mitandao yote ya kijamii: @tmcnewsmedia
#TMCNews #ShapingTheFuture #BreakingNews #TanzaniaNews #LiveNews#TMCNews #Dodoma #MailiMbili #Ostabei #UsalamaWaRaia #PolisiTanzania #HabariZaTanzania #ShapingTheFutureTMC