HECHE ATOA MSIMAMO WA CHADEMA KUHUSU KATIBA MPYA
MISALABA MEDIA
0:00 / 0:00
HECHE ATOA MSIMAMO WA CHADEMA KUHUSU KATIBA MPYA
6 760 просмотров · 10 ч назад
MISALABA MEDIA
23,7 тыс. подписчиков
6 760 просмотров · 10 ч назад
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, John Heche, amesisitiza umuhimu wa Tanzania kupata Katiba mpya, akieleza kuwa suala hilo ni muhimu katika kujenga misingi bora ya uongozi na maendeleo ya wananchi.
Heche ameyasema hayo leo, Septemba 22, 2026, wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Uwanja wa Jasko, Kata ya Ngokolo, Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katika mkutano huo, Heche pia amesisitiza umuhimu wa Serikali kufufua viwanda vilivyopo nchini ili kuongeza fursa za ajira na kuwawezesha wananchi, hususan wazawa, kunufaika na fursa za kiuchumi zinazotokana na uwekezaji na uzalishaji.
Amesema kufufuliwa kwa viwanda kutasaidia kuongeza uzalishaji wa bidhaa nchini pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi na maendeleo ya wananchi.