Перейти к содержимому

Umata Yatoa Huduma Ya Chakula Hospitali Ya Malawi Yombo Vituka Wilaya Ya Temeke 3 July 2026

Khidmatul-Ummah Official (خدمة الأمة)

0:00 / 0:00

Umata Yatoa Huduma Ya Chakula Hospitali Ya Malawi Yombo Vituka Wilaya Ya Temeke 3 July 2026

54 просмотра · 3 месяца назад
Khidmatul-Ummah Official (خدمة الأمة)
1,26 тыс. подписчиков
54 просмотра · 3 месяца назад
UMATA YAWAFIKIA WAGONJWA KWA HUDUMA YA CHAKULA – HOSPITALI YA MALAWI, YOMBO VITUKA, DAR ES SALAAM – 3 JULY 2026 Taasisi ya UMATA (Umoja wa Maimamu na Walimu wa Madrasa Tanzania) imetoa huduma ya chakula kwa wagonjwa, ndugu na walezi wao pamoja na wahudumu wa Hospitali ya Malawi, Yombo Vituka, Dar es Salaam. Huduma hiyo imelenga kuwafariji wagonjwa, kuwatia moyo ndugu na walezi wao, pamoja na kuimarisha utamaduni wa huruma na kusaidiana katika jamii. Walionufaika na huduma hiyo ni: • Wagonjwa • Ndugu na walezi wa wagonjwa • Wahudumu wa hospitali قال رسول الله ﷺ: «مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيَا نَفَّسَ اللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ الْقِيَامَةِ» "Atakayemuondolea Muumini dhiki katika dhiki za dunia, Mwenyezi Mungu atamuondolea dhiki katika dhiki za Siku ya Kiyama." (Imepokewa na Muslim) Zoezi hili limefanyika chini ya uongozi makini wa Sheikh Arif Surya, Sheikh Yahya Mkumba, Abuu Ayman, Sheikh Amir Mbwana, Dr. Kamna, Abuu Hafsa, Juma Mwira, pamoja na viongozi na wajumbe wengine wa UMATA kwa nafasi zao mbalimbali. Mungu aibariki Taasisi ya UMATA, wafadhili na wote wanaoshiriki katika kuwahudumia wenye uhitaji.