KWANINI YESU ALILIA HALI WATU ALIOWAONEA HURUMA WALIIMBA HOSANA?
Gwakisa Mwaipopo
0:00 / 0:00
KWANINI YESU ALILIA HALI WATU ALIOWAONEA HURUMA WALIIMBA HOSANA?
70 просмотров · 1 год назад
Gwakisa Mwaipopo
29,1 тыс. подписчиков
70 просмотров · 1 год назад
Kwanini Yesu Alilia Hali Watu Waliimba Hosana?
Yesu aliingia Yerusalemu akipokelewa kwa shangwe na vigelegele vya "Hosana!"—lakini badala ya kufurahia, aliutazama mji na kulia. Kwa nini?
Katika episode hii ya kina, tunachambua sababu ya kilio cha Yesu katikati ya kelele za sifa. Tunagundua kwamba, Yerusalemu ilikuwa na sauti ya ibada, lakini moyo wake ulijaa uovu, unafiki wa kisiasa, na mfumo wa kidini uliogeuka kuwa pango la wanyang'anyi. Hili linaakisi hali ya kizazi chetu leo: makanisa mengi, sifa nyingi, lakini mioyo iliyopoteza mwelekeo wa Mungu.
🕊️ Yesu hakushawishika na Hosana za watu—alilia kwa sababu aliona mbali zaidi ya kelele zao. Aliona maangamizi yanayokaribia, moyo wa taifa lililojifunika kwa dini bila toba, na watu waliomkaribisha kwa midomo lakini wakamkana kwa moyo.
📌 Tazama au sikiliza tafakari hii ili ujifunze:
Jinsi dhambi hujificha ndani ya mfumo wa ibada
Hatari ya mafanikio bila mizizi ya ufunuo
Na kwanini kila mmoja wetu ana “Yerusalemu” anayopaswa kujiandaa kuikabili
🔔 Usisahau kusubscribe, kushiriki, na kufuatilia Voice of Hope kwa mafundisho ya kweli yasiyogoshiwa.
#KablaYaHosana #VoiceOfHopePodcast #HosanaBilaUfunuo #YerusalemuYaLeo #KilichomlizaYesu #SautiYaKusudi #PodcastYaKiroho #AmkaNaKweli