KADOGOSA: MBAUDA–ARUSHA BYPASS IKAMILIKE DESEMBA 2026
Wizara ya Ujenzi
0:00 / 0:00
KADOGOSA: MBAUDA–ARUSHA BYPASS IKAMILIKE DESEMBA 2026
2 370 просмотров · 1 дн. назад
Wizara ya Ujenzi
9,28 тыс. подписчиков
2 370 просмотров · 1 дн. назад
Waziri wa Ujenzi, Mhe. Masanja Kadogosa, amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha–Kibaya–Kongwa, sehemu ya Mbauda–Losinyai na Tanganyika Packers–Losinyai yenye urefu wa kilometa 70, kuhakikisha kipande cha Kona ya Mbauda–Arusha Bypass kinatekelezwa kwa mujibu wa mkataba na kuzingatia viwango na ubora unaotakiwa.
Waziri Kadogosa ametoa agizo hilo jijini Arusha, Oktoba 6, 2026, wakati akikagua barabara zinazojengwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 ambapo Ukaguzi huo umefanyika katika maeneo ya Mbauda, Mushono na Kwa Mromboo.
Akiwa katika eneo la Mbauda, Waziri Kadogosa amepongeza maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo, akieleza kuwa kilometa 13 zimepewa kipaumbele maalum katika maandalizi ya AFCON 2027.