Перейти к содержимому

VIONGOZI WA KANISA JIMBO LA MBEYA MAGHARIBI WAASWA KUWEKEZA KWA WATOTO/ WITO NA MWL. LUGANO NDILIE

ELCT KONDE TV

0:00 / 0:00

VIONGOZI WA KANISA JIMBO LA MBEYA MAGHARIBI WAASWA KUWEKEZA KWA WATOTO/ WITO NA MWL. LUGANO NDILIE

20 просмотров · 2 ч назад
ELCT KONDE TV
3,04 тыс. подписчиков
20 просмотров · 2 ч назад
VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUWEKEZA KWA VIJANA NA WATOTO Viongozi wa dini, wakiwemo wachungaji na wainjilisti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Konde, Jimbo la Mbeya Magharibi, wametakiwa kuwekeza zaidi katika malezi na makuzi ya watoto na vijana, kwa kuwajenga katika misingi ya Neno la Mungu ili kuwa watumishi bora wa kizazi kijacho. Wito huo umetolewa na Mwalimu wa Neno la Mungu Lugano Ndile wakati wa Mafundisho ya Biblia Kwa wachungaji na wainjilisti ambapo Ndile amewasihi viongozi hao kutimiza wajibu wao wa kuwekeza Katika Malezi Bora Kwa vijana na watoto kwa kuzingatia mafundisho ya Neno la Mungu. Kwa upande wake, Mkuu wa Jimbo la Mbeya Magharibi, Mchungaji Nancy Maro, amewasihi wachungaji na wainjilisti kuyafanyia kazi mafundisho yote waliyopokea, huku akisisitiza umuhimu wa kufuatilia kwa karibu ufundishaji wa masomo ya Biblia kwa watoto. Nao baadhi ya wachungaji na wainjilisti walio hudhuria mafundisho hayo kutoka katika sharika mbalimbali za KKKT Jimbo la Mbeya Magharibi, wameeleza namna walivyopokea mafundisho hayo na umuhimu wake katika kuboresha huduma kwa watoto na vijana.