Ubungo, Kinondoni waanza kuondoa magari yaliyochakaa barabarani
TBConline
0:00 / 0:00
Ubungo, Kinondoni waanza kuondoa magari yaliyochakaa barabarani
397 просмотров · 6 дней назад
TBConline
525 тыс. подписчиков
397 просмотров · 6 дней назад
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na Kinondoni jijini Dar es Salaam zimeanza zoezi la kuondoa magari yaliyochakaa barabarani, vyuma chakavu na shughuli za gereji pembezoni mwa barabara za mitaa ya manispaa hizo.
Zoezi hilo linakuja ikiwa katika hali ya kujiandaa kukabiliana na mvua za msimu wa vuli za juu ya wastani zinazoathiriwa na hali ya El Nino zinazotarajiwa kuanza kunyesha hapa nchini katika wiki ya nne ya mwezi Septemba katika ukanda wa ziwa Victoria na kuenea maeneo mengine wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba.
Kamera ya TBC Digital imeshuhudia mabango yakiwekwa kutahadharisha watu kutofanya shughuli yoyote pembezoni mwa barabara.
Wakati huo huo katika mitaa ya Tandale mkoani humo, Wakuu wa Wilaya hizo hawakuwa nyuma katika kuhakikisha zoezi linakwenda sawa bila changamoto yoyote.
Ikumbukwe, mwezi Agosti mwaka huu Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) ilitoa tahadhari ya kuwepo kwa msimu wa mvua za vuli unaotarajiwa kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Niño yenye nguvu kubwa, hivyo mvua za Juu ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi ikiwemo Ukanda wa Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, Ukanda wa Ziwa Victoria na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.