KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING | 13 AUGUST 2026
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
0:00 / 0:00
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING | 13 AUGUST 2026
4 859 просмотров · Трансляция закончилась 2 недели назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
63,7 тыс. подписчиков
4 859 просмотров · Трансляция закончилась 2 недели назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING | 13 AUGUST 2026
UJUMBE WA LEO:
MGEUKO WA FIMBO YA HARUNI
HARUSI YA KANA YA GALILAYA NA NGUVU YA MGEUKO KATIKA KUWEZEKANA
Kutoka Fimbo Kavu Mpaka Ushahidi wa Matunda
Hesabu 16 : 1 - 35
Hesabu 17 : 1 - 8
Yeremia 1 : 11 - 12
Kuna jambo kubwa sana ndani ya fimbo ya Haruni Mungu hakutumia fimbo iliyokuwa tayari inachanua; alichukua fimbo iliyokuwa imekauka na kuifanya iwe ushahidi wa nguvu zake.
Fimbo hiyo ilikuwa imehusishwa na mamlaka, vita, mapigo na miujiza, lakini ilipowekwa mbele za Bwana, Mungu aliionyesha katika sura nyingine ikachipua, ikachanua na kuzaa matunda.
Hapa ndipo tunapoona mgeuko wa neema:
Mungu anaweza kuchukua kile kilichoonekana kimefika mwisho na kukifanya kuwa ushahidi wa mwanzo mpya.
JAMBO LA KUJIFUNZA LA KWANZA: MUNGU ANAWEZA KUTUMIA KILE KILICHOKAUKA
Fimbo ya Haruni haikuwa mti hai. Ilikuwa fimbo imekatwa kutoka kwenye chanzo chake na kwa hali ya kawaida haikuwa na uwezo wa kuendelea kukua.
Hii ni picha ya mtu ambaye amepitia misimu ambayo imeonekana kumaliza nguvu zake.
Watu wanaweza kuangalia maisha yako na kuona:
“Huyu amekauka.”
“Huyu amepoteza nafasi yake.”
“Huyu hawezi tena kuzaa.”
Lakini Mungu haangalii tu hali uliyonayo; anaangalia kile neema yake inaweza kufanya kupitia wewe.
Usijitambulishe kwa ukavu wako wa sasa.
Kuna tofauti kati ya kile ulicho nacho leo na kile Mungu anaweza kufanya kupitia wewe kesho.
Fimbo inaweza kuwa kavu, lakini kusudi la Mungu juu yake halijakauka.
]JAMBO LA KUJIFUNZA LA PILI: MAMLAKA YA KWELI HUTHIBITISHWA KWA MATUNDA
Cheo kinaweza kutajwa kwa kinywa, lakini matunda ndiyo yanayotoa ushahidi wa kile Mungu ameweka ndani yako.
Fimbo haikusema,
“Mimi ni ya Haruni.”
Ilichanua.
JAMBO LA KUJIFUNZA LA TATU: MGEUKO MKUBWA HUANZA KATIKA SIRI NA MUNGU
Fimbo haikuchanua mbele ya umati.
iliwekwa mbele za Bwana
katika Hema la Ushuhuda.
Kabla ya Mungu kukuthibitisha hadharani, anaweza kukutengeneza kwa siri.
Kuna misimu ambayo hakuna anayekuona.
Hakuna anayejua Mungu anafanya nini ndani yako.
Unaweza kuona kama maisha yako yamesimama, lakini kumbe Mungu anafanya kazi ambayo macho ya watu hayawezi kuona.
Ndiyo maana usiogope:
Msimu wa kimya, msimu wa kutokujulikana, Msimu wa kusubiri,
Msimu ambao hakuna anayekushangilia.
Mhubiri: Reinhard Mlawi
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com