Перейти к содержимому

MWANAFUNZI ASIYEONA AIBEBA NYANDA ZA JUU KUSINI TUZO ZA BMT 2026

Makutano TV

0:00 / 0:00

MWANAFUNZI ASIYEONA AIBEBA NYANDA ZA JUU KUSINI TUZO ZA BMT 2026

226 просмотров · 3 месяца назад
Makutano TV
4,21 тыс. подписчиков
226 просмотров · 3 месяца назад
Kipaji ni uwezo wa asili wa kufanya jambo kwa urahisi, ubunifu, na kiwango cha juu cha ubora bila kuhitaji nguvu nyingi. Hapa ni Shule jumuishi ya Msingi Kipera Mara hii tumerudi hapa Kipera, Iringa vijijini, kwa sababu moja tu, kusheherekea mafanikio ya kipaji Exaud Paul Lugenge mwanafunzi wa Shule hii. ndiye aliyetwaa tuzo ya mwanamichezo bora wa kiume mwenye ulemavu tuzo zilizotolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) msimu wa 4, zilizotolewa jijini Dar es salaam Mei 9, 2026 Exaud mwenye umri wa miaka 16, mtoto wa pili kuzaliwa katika familia ya watoto 5, hivi sasa yupo darasa la 7 akisoma pamoja na dada yake ambaye pia anachangamoto ya kuona, wote ni wachezaji mahiri wa mpira wa goli (ama Goal Ball). Ndoto ya Exaud ni kuwa mchezaji mkubwa duniani katika mchezo huu wa goli Watoto wenye ulemavu wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa fursa za michezo kutokana na unyanyapaa, miundombinu mibovu, na uhaba wa vifaa maalum. Changamoto hizi huwanyima haki yao ya kushiriki na kufaidika na michezo, pembeni ya mafanikio haya wapo wadau IBO Italia. Bila shaka Tuzo hizi za EXaud tunaweza kusema zimekuja kama wito kwa Wazazi, Serikali, wadau, waalimu na jamii yote, na tunaamini itachochea msukumo wa utekelezaji wa sera katika elimu, michezo na maisha jumuishi. Swali ni hili kwako mtazamaji …ni nini kikwazo cha kipaji kwa mtoto wako? je ni ulemavu? ni eneo la michezo? ni vifaa? Exaud kavuka vikwazo vyote hivi, na kudhihirisha kwamba hakuna kiwezacho kuzuia kipaji #IBO #BMT #WAZIRI WA HABARI MICHEZO NA UTAMADUNI #childprotection