Перейти к содержимому

Welcome To Sauti Ya Huruma Podcast

Sauti Ya Huruma Podcast

0:00 / 0:00

Welcome To Sauti Ya Huruma Podcast

481 просмотр · 2 нед. назад
Sauti Ya Huruma Podcast
347 подписчиков
481 просмотр · 2 нед. назад
Kuna upande wa Baba yetu Rev.Dr.Huruma Nkone ambao huwezi kuujua kwa kumuona madhabahuni peke yake. Umesikia mafundisho yake. Umeona huduma yake. Umeona kile kinachoonekana hadharani. Lakini safari hii, tunakualika uone zaidi ya hapo. Karibu kwenye mazungumzo yanayokwenda zaidi ya madhabahu. Katika safari hii, Baba yetu Rev.Dr.Huruma Nkone atakutana na wanaume na wanawake waliobeba hekima, uzoefu na ushawishi katika imani, uongozi, biashara na ujenzi wa Ufalme wa Mungu. Hapa ni mahali ambapo uzoefu unageuka kuwa hekima.Ambapo maswali yanazaa ufunuo.Ambapo imani inakutana na uongozi.Na ambapo masomo ya safari ya maisha yanawekwa mezani kwa kizazi kinachokuja. Na labda kwa mara ya kwanza, utapata kumjua mchungaji nje ya madhabahu, kupitia mawazo yake, maswali yake, maono yake na mazungumzo ambayo kwa kawaida huyapati hadharani. Hiki unachokiona ni mwonekano mdogo tu wa kile kinachokuja. Hii ni safari ambayo unahitaji kuwa sehemu. Jiandae.