UKWELI KIFO CHA MKE ALIYEPIGWA RISASI/ JENI ALITABIRI KIFO CHAKE? DADA AFICHUA HOFU YATANDA
Mwananchi Digital
0:00 / 0:00
UKWELI KIFO CHA MKE ALIYEPIGWA RISASI/ JENI ALITABIRI KIFO CHAKE? DADA AFICHUA HOFU YATANDA
21 104 просмотра · 3 дня назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
21 104 просмотра · 3 дня назад
Bella Urassa, dada wa marehemu Jenipher (Jeni) Urassa amesema mdogo wake alimweleza siku chache kabla ya kuuawa kuwa alikuwa na hofu kuhusu usalama wa maisha yake, akihusisha hofu hiyo na mgogoro wa umiliki wa nyumba yao iliyopo Bunju, Dar es Salaam.
Bella amesema Jeni alimweleza kuwa hati ya nyumba hiyo ilitoka ikiwa na majina ya watoto wao wanne, huku yeye akiwa msimamizi wao, jambo ambalo alidai lilipingwa na mume wake aliyekuwa akitaka hati hiyo iandikwe kwa majina ya wanandoa hao. Kwa mujibu wa Bella, baada ya hati hiyo kutoka, Jeni aliwahi kusema anaamini mume wake angeweza kumuua.
Jeni, mzaliwa wa Nkuu Sinde, Kata ya Machame Mashariki, Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, anadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na mume wake alfajiri ya Alhamisi, Oktoba Mosi, 2026, nyumbani kwao Bunju, baada ya kutokea kwa tafrani ndani ya chumba walichokuwa wakiishi.
Bella amesema kabla ya kifo chake, Jeni alikuwa ameondoka nyumbani na kukaa kwa ndugu yake kwa takribani miezi miwili kutokana na mgogoro wa kifamilia. Hata hivyo, siku moja kabla ya kifo chake alikwenda nyumbani kuwaona watoto na kuwapelekea chakula alichotumiwa kutoka Nkuu Sinde. Badala ya kurejea kwa ndugu yake, alilala nyumbani na watoto, wakati mume wake akiwa Moshi.
Akizungumzia mazishi, baba mdogo wa marehemu, Joseph Urassa, amesema familia ya kwao imeamua kumzika Jeni nyumbani kwao, kama alivyokuwa ameomba, katika makaburi ya Usharika ambako baba yake alizikwa. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa ukoo wa familia alikoolewa, Mchungaji Tumsifu Kweka, amesema familia yao haitalumbana na familia ya Urassa na itaheshimu taratibu zitakazokubalika kuhusu mahali marehemu atakapozikwa.
Kwa undani wa Mahojiano haya, tazama kupitia YouTube ya Mwananchi Digital.