PST. EZEKIEL AZUNGUMZIA KUHUSU SWALA LA WEMA SEPETU.
Chomoza Digital
0:00 / 0:00
PST. EZEKIEL AZUNGUMZIA KUHUSU SWALA LA WEMA SEPETU.
14 840 просмотров · 3 месяца назад
Chomoza Digital
10,1 тыс. подписчиков
14 840 просмотров · 3 месяца назад
Baada ya watu wengi kuhusisha ushuhuda wa kupata mtoto wa Wema Sepetu na maombi aliyowahi kuombewa na Mtumishi wa Mungu Pst. Ezekiel. Sasa kwa mara ya kwanza kupitia Chomoza Media Mtumishi huyu wa Mungu kutoka Kenya, Pst. Ezekiel, amezungumzia jambo hilo hadharani.
Kwa unyenyekevu, amesema wazi kwamba yeye hakumpa mtoto Wema Sepetu, bali ni Mungu pekee ndiye anayestahili sifa na utukufu kwa kile kilichotokea. Ameeleza kuwa watumishi wa Mungu ni vyombo tu vinavyotumiwa na Mungu, lakini mwenye kufanya miujiza na kujibu maombi ni Mungu mwenyewe.
Kauli hiyo imekuwa ukumbusho muhimu kwamba imani yetu isiwekwe kwa wanadamu, bali kwa Mungu ambaye ndiye chanzo cha baraka zote. Na amesisitiza kuwa Swala la Uponyaji huwa alihusiani na Dini bali Imani ya Mtu mwenye uhitaji. Hakika, Mungu bado anatenda leo, na wakati wake ni mkamilifu.