PAMBANIA UHAI
Dandu Malagha
0:00 / 0:00
PAMBANIA UHAI
185 просмотров · 8 дней назад
Dandu Malagha
423 подписчика
185 просмотров · 8 дней назад
Kipo kipindi ambacho mwili unahitaji huduma za afya kutokana na magonjwa, na hapo ndipo tunahitaji msaada na michango kutoka kwa wengine. Hata hivyo, badala ya kufanya hivyo, binadamu wengi wamegeuza jambo hili kuwa kama fasheni ya kuonekana kwenye misiba. Watu wanaweza kupata taarifa kwamba mtu fulani anaumwa, lakini usiwaone wakimtembelea au kumsaidia. Inapotokea mtu huyo amefariki, wengi huona ni muhimu zaidi kwenda msibani kuliko kumsaidia wakati wa ugonjwa wake.
Michango mingi huonekana zaidi wakati wa misiba kuliko wakati wa matatizo ya kiafya. Makundi mengi yameundwa kwa kuzingatia matukio ya misiba, lakini si kusaidia wagonjwa. Hata katiba za baadhi ya makundi mbalimbali zimeweka kando au hazijazingatia kabisa huduma za kusaidia wanachama wanapougua.
Wimbo huu unatukumbusha kwamba mwili wa mwanadamu peke yake hauna thamani kubwa baada ya kifo; thamani yake kubwa ipo wakati mtu akiwa hai. Ndiyo maana tunapaswa kuonyesha upendo, huruma, na msaada wetu kwa watu wanapouhitaji zaidi wakiwa bado hai, badala ya kusubiri hadi wanapofariki.
English Translation
There comes a time when the human body needs medical care due to illness, and that is when support and contributions from others are most needed. Unfortunately, instead of doing so, many people have turned this into a social fashion of being seen at funerals. People may hear that someone is seriously ill, yet very few take the time to visit or assist them. However, when that person passes away, many suddenly find it important to attend the funeral rather than having supported them during their illness.
Most contributions and fundraising efforts are seen during funerals rather than during times of sickness. Many groups and associations have been established with provisions for funeral support, but not for assisting members when they are ill. In fact, the constitutions of many organizations either exclude or give little attention to support for members facing health challenges.
This song reminds us that the human body alone holds little value after death; its greatest value exists while a person is still alive. Therefore, we should show love, compassion, and support to people when they need it most—while they are still living—rather than waiting until they have passed away.