Перейти к содержимому

Dawasa yaweka uangalizi maeneo 20 kukabili El- Nino

Mwananchi Digital

0:00 / 0:00

Dawasa yaweka uangalizi maeneo 20 kukabili El- Nino

192 просмотра · 3 дня назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
192 просмотра · 3 дня назад
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) imeweka uangalizi maalumu katika maeneo 20 ya miundombinu ya maji ili kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El- Nino. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mkama Bwire, amesema maeneo hayo yanahusisha vyanzo vya maji, mitambo ya uzalishaji, mabomba makubwa ya kusafirisha maji na mifumo ya majitaka. Amesema mamlaka hiyo imefanya tathmini kubaini maeneo yenye hatari kubwa ya mafuriko na mmomonyoko wa ardhi, huku hatua za kuimarisha kingo za mito na kulinda mabomba zikichukuliwa. Bwire amesema maeneo ya Mto Mpiji, Selander Bridge na Jangwani ni miongoni mwa maeneo yanayopewa uangalizi kutokana na historia ya kuathiriwa na mafuriko. Amesema Dawasa pia imeweka vifaa vya dharura, ikiwamo mabomba ya maji ili kurahisisha urejeshaji wa huduma endapo miundombinu itaharibika.