Mwongozo wa Kujifunza Biblia || Somo la 7 || Tatizo la Uovu || Sabato Mchana || 1Q2025
The Gospel Media
0:00 / 0:00
Mwongozo wa Kujifunza Biblia || Somo la 7 || Tatizo la Uovu || Sabato Mchana || 1Q2025
238 просмотров · 1 год назад
The Gospel Media
9,45 тыс. подписчиков
238 просмотров · 1 год назад
Hili si tatizo la kitaaluma tu bali ni jambo ambalo linasumbua sana watu wengi na linalowazuia wengine kumjua na kumpenda Mungu.
“Kwa akili za watu wengi chimbuko la dhambi pamoja na sababu ya kuwepo kwake ni jambo linalotatanisha sana. Wanaona kazi ya uovu na matokeo yake ya kutisha ya huzuni na taabu, na wanahoji ni kwa jinsi gani haya yote yaweza kuwepo chini ya utawala wa Mungu ambaye hana kikomo katika hekima, nguvu na upendo. Hapa kuna siri ambayo hawana maelezo yake.”—Ellen G. White, Pambano Kuu, Uk 406
Wakanamungu wengi hutambua tatizo la uovu kama sababu ya wao kuwa wakanamungu. Lakini kama tutakavyoona katika juma hili na katika majuma yanayokuja, Mungu wa Biblia ni mwema kabisa, na tunaweza kumtumaini—hata licha ya uovu unaoathiri ulimwengu wetu ulioanguka.