SOLO THANG: HUYU AFANDE SELE SIO MFALME WA RHYMES,HAJUI ANAANDIKA HOTUBA TU
MABENA TV
0:00 / 0:00
SOLO THANG: HUYU AFANDE SELE SIO MFALME WA RHYMES,HAJUI ANAANDIKA HOTUBA TU
4 660 просмотров · 2 дня назад
MABENA TV
114 тыс. подписчиков
4 660 просмотров · 2 дня назад
#Solothang #afandesele #rhymes
SOLO THANG AMCHANA AFANDE SELE: AMTAKA ATHIBITISHE UFALME WA RHYMES! 🎤
Mapema leo, mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, @solothang_aka_ulamaa , ametoa kauli inayoweza kuibua mjadala miongoni mwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva, akizungumzia madai ya @afandeselemorogoro kuendelea kujitambulisha kama Mfalme wa Rhymes.
Solo Thang ameeleza kuwa kujisifia mara kwa mara kwa kutumia jina hilo hakutoshi, bali Afande Sele anatakiwa kurudi studio, kutengeneza nyimbo kali na kushirikiana na wasanii wa kizazi kipya ili kuonyesha uwezo wake kupitia kazi zake.
Aidha, Solo Thang amedai kuwa Afande Sele anapaswa kutumia muziki wake kuthibitisha kwa mashabiki kwamba bado anastahili heshima ya kuitwa Mfalme wa Rhymes, badala ya kutegemea jina hilo pekee.
Je, unakubaliana na kauli ya Solo Thang, au unaamini Afande Sele anastahili kuendelea kuitwa Mfalme wa Rhymes kutokana na historia na mchango wake katika muziki wa Hip Hop nchini?