WAHITIMU WA ETE KKKT CATHEDRAL MTWARA WATUNUKIWA VYETI NA KUINGIZWA KAZINI.
NGAO MEDIA
0:00 / 0:00
WAHITIMU WA ETE KKKT CATHEDRAL MTWARA WATUNUKIWA VYETI NA KUINGIZWA KAZINI.
301 просмотр · 4 мес. назад
NGAO MEDIA
1,78 тыс. подписчиков
301 просмотр · 4 мес. назад
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Kusini Mashahariki, limehitimisha mafunzo ya wanafunzi wa Theolojia elezi ETE kwa kuwapatia vyeti wanafunzi 40 waliohitimu pamoja kuwaingiza kazini.
Akihubiri katika ibada iliyofanyika katika Usharika wa Cathedral na Kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali,wakiwepo Wachungaji,Wakuu wa Majimbo na Wasaidizi wa Maaskofu,Msaidizi wa Askofu Dayosisi wa Kusini Njombe DAKT.JOHNSON GUDAGA amewataka wahitimu hao kutohubiri Injili kwa mazoea, badala yake wamshirikishe Roho Mtakatika na kusaidiana katika Utumishi wao.
Ibada hiyo pia imeambatana uzinduzi wa Kitenge cha Dayosisi na Tisheti za UKWATA, ambapo Askofu wa KKKT DKMSH YERIKO NGWEMA ameongoza zoezi hilo na kutoa Neno kwa Kanisa.
Aidha Mkurugenzi wa ETE Ukanda wa Kusini Mchungaji ELIA KONGA, amesema licha ya changamoto zilizipo wanafunzi 40 kati ya 60 wamefanikiwa kuhitimu mafunzo hayo,huku akitoa wito kwa washarika wengine kujiunga na Eelimu hiyo bila kujali umri wao.
Nao baadhi ya viongozi kutoka maeneo mbalimbali akiwepo Mchungaji Mtaafu STEPHANO kutoka Swiden,ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya SEM,na Msaidizi wa Askofu Dira iliyopo Mkoani Iringa ZAKARIA MGEYEKWA wa huduma ya Uinjilist kwa Wafugaji na Wavuvi MUWA wameeleza namna wanavyofanya kazi ya MUNGU katika maeneo mbalimbali.