Перейти к содержимому

KUMBUKUMBU YA MWALIMU JOHN S. MGANDU: Mtunzi mahiri wa muziki mtakatifu kanisa katoliki – Tanzania

Amatha K. Mwapinga(Beloved)

0:00 / 0:00

KUMBUKUMBU YA MWALIMU JOHN S. MGANDU: Mtunzi mahiri wa muziki mtakatifu kanisa katoliki – Tanzania

16 020 просмотров · 3 года назад
Amatha K. Mwapinga(Beloved)
2,95 тыс. подписчиков
16 020 просмотров · 3 года назад
Documentary, John S. Mgandu: Mtunzi, organist na Mwalimu wa muziki Mtakatifu Kanisa Katoliki -Tanzania TAIFA LA MUNGU TUMSIFU YESU KRISTO Naamini tutajifunza kitu, kupitia hiki kidogo nilicho andaa kwa ajili ya kumkumbuka na kumuenzi mwl. wetu mpendwa aliyefariki Tar. 10/07/2008. Sikubahatika kufanya utume pamoja naye kwa muda mrefu, hivyo nimeandaa kitu kidogo sana kwa ruhusa ya familia. Tumuombee mwl. wetu pumziko la amani na la milele. Amatha K. Mwapinga, mwanakwaya na mwandaaji wa Documentary za video YEYE BINAFSI, kuhusu watunzi wa muziki mtakatifu Kanisa Katoliki Tanzania. Vilevile anajihusisha na kufundisha mada mbalimbali kuhusu wana utume na utume wa uimbaji. Mwaka 2022 aliandaa Documentary ya Kwanza fupi kumhusu mtunzi mahiri wa muziki mtakatifu, mwl. John Stephano Mgandu, kwa gharama zake mwenyewe bila kupata msaada wowote toka kwa mtu au kikundi. Alianza rasmi kazi hii mwezi July 2022 na kuikamilisha mwezi October 2022. Baadhi ya walioshiriki kutoa ushauri katika kazi hii ni Askofu Eusebius Nzigilwa, Stephano Mgandu Maganga(Mtoto wa marehemu Mwl. J. Mgandu) na walimu wawili wa muziki mtakatifu ambao ni Dr. Shanel Komba na Alex Manyama. Kazi hii ilikaguliwa na kupitishwa na Fr. Dr. Joseph Peter Mosha, Paroko wa Parokia ya chuo kikuu(UDSM) na nakala kukabidhiwa Kanisa Katoliki Tanzania(TEC) kupitia Mkurugenzi wa litrujia Pd. Stefano Kaombe. ‪@KANISAKATOLIKITANZANIATEC‬ ‪@tumainitelevision‬ ‪@RadioMariaArgentina‬ ‪@radiomariatanzania‬ @radiomaria