Перейти к содержимому

ZIJUE AHADI ZA MUNGU KWAKO | SIRI ILIYOPO KWENYE AHADI ZA MUNGU AGANO LA KALE / AGANO JIPYA | FAHAMU

CHARISMA TV

0:00 / 0:00

ZIJUE AHADI ZA MUNGU KWAKO | SIRI ILIYOPO KWENYE AHADI ZA MUNGU AGANO LA KALE / AGANO JIPYA | FAHAMU

2 497 просмотров · 3 года назад
CHARISMA TV
3,01 тыс. подписчиков
2 497 просмотров · 3 года назад
AHADI ZA MUNGU KWAKO NI ZIPI ?.. Watu wengi hawazitumii ahadi za Mungu; yaani kudai haki zao kupitia ahadi za zake. Kuna ahadi za Mungu nyingi sana zaidi ya 7147 kwenye Biblia. Kwanzia Agano la Kale mpaka Agano Jipya. Kwa anayejua kuzitumia ahadi za Mungu ananufaika sana maana Mungu hajipingi. Lolote analozungumza ni lazima alitimilize. Ahadi za Mungu ni yale yote ambayo Mungu ameyazungumza kuhusiana na sisi. Yote ambayo Mungu amezungumza katika namna ya kutupatia na kututendea hizo zote ni ahadi zake. Zipo ahadi za Mungu ambazo zilizungumzwa kwenye AGANO LA KALE na AGANO JIPYA. Wengi wanadhani ahadi za Mungu zipo agano la kale tu; lakini pia hata agano jipya zipo ahadi za Mungu. Mfano, Mathayo 7:7 hii ni ahadi ya kuomba na kupewa, Mathayo 6:33, nayo hii pia ni ahadi ambayo kuna kuzidishiwa pale ambapo mtu amepata ufalme wa Mungu. Hivyo unao uhakika wa wewe kudai ahadi hii. Ahadi za Mungu zina nguvu sana. Kila ambacho Mungu amezungumza juu yako utimilifu wake upo ndani ya Kristo Yesu,yaani kinaweza kutimilika na kukamilika. Kwa maana ipo nguvu ya kufanya chochote ambacho Mungu amekizungumza kinachokuhusu wewe kikakamilika kupitia Yesu Kristo. Isaya 43:26 Mungu anataka kukumbushwa; sio kwamba anataka akumbushwe kwa sababu anasahau la hasha! Mungu anataka kukumbushwa ili kuona umakini wako,kwamba upo makini kiasi gani kujua haki zako za msingi ni zipi. Kuna haki zako inabidi ukumbushe ili upewe. Maana yake usipokumbusha kuna vitu unaweza usiwe navyo. Isaya 41:21 Ingawa Mungu anafahamu unataka nini lakini anataka kusikia. Nguvu ya uwezeshaji wa jambo lolote la kiungu upo katika maneno ndiyo maana chochote unachokiona Mungu alikifanya kwa neno. Ni lazima uwe na ushahidi wa kumwambia Mungu kuwa hapa ulisema hivi na hivi na maombi mazuri ni yale yanayobebwa na NENO LA MUNGU. 2Wakorintho1:20 Ili Mungu apate kutukuzwa kwa sisi ni lazima tunapozitamka ahadi za Mungu katika Kristo Yesu zitii yale yaliyoahidiwa maana ahadi za Mungu ni NDIYO katika Kristo Yesu. Je unaitaji kujifunza zaidi piga +255 682 599 376 #ProphetSimonCharisma #charismageneration #kizazikilichokataakufa #kizazikinachoishimilele #tunaishimpakaunyakuo #uzimanamafanikio CLICK THE "SUBSCRIBE BUTTON" on the bottom right corner of the video. Follow Us On: INSTAGRAM:   / prophetsimoncharisma   FACEBOOK:   / prophetsimoncharisma   #LCM2023 #UzimanaMafanikio #charismatv #sundayservice #love #prayer #pray #hope #bible #jesuschrist #christian #faith #jesus #motivation #christ #gospel #meditation #truth #christianity #worship #believe #holyspirit #spirituality #healing #charismageneration #kizazikilichokataakufa #kizazikinachoishimilele #tunaishimpakaunyakuo #uzimanamafanikio #scripture #spiritual #grace #loveyourself #amen #prophetic worship #Haleluya Tv #prophetic fire #propheticanddeliverance #propheticandhealingministry #tanzania #kenya #uganda