KAMATI YA SIASA NJOMBE YARIDHISHWA NA UJENZI WA DARAJA LA MAWE LA KM 6.35 RAMADHANI
NJOMBE TC
0:00 / 0:00
KAMATI YA SIASA NJOMBE YARIDHISHWA NA UJENZI WA DARAJA LA MAWE LA KM 6.35 RAMADHANI
101 просмотр · 4 недели назад
NJOMBE TC
670 подписчиков
101 просмотр · 4 недели назад
KAMATI YA SIASA NJOMBE YARIDHISHWA NA UJENZI WA DARAJA LA MAWE RAMADHANI
Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Njombe imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa Daraja la Mawe lenye urefu wa kilomita 6.35 katika eneo la Ramadhani, likielezwa kuwa litakuwa suluhisho la changamoto ya usafiri kwa wananchi pamoja na kuongeza fursa za utalii katika eneo hilo.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua mradi huo, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Okoka, amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa ujenzi huo, akibainisha kuwa ukubwa na muundo wa daraja hilo unaweza kulifanya kuwa kivutio cha utalii.
Amesema kukamilika kwa mradi huo kutarahisisha usafiri na shughuli za kiuchumi kwa wananchi, huku likitoa fursa ya kulitangaza eneo hilo kama sehemu ya vivutio vya utalii.
Kamati hiyo imesisitiza umuhimu wa kuendelea kusimamia ubora na kasi ya ujenzi ili daraja hilo likamilike kwa wakati na kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi.