MAPENZI NI MHIMU ILIA UKIONA MAPENZI HAYAPO CHUKUA HATUA ZA KISHERIA SIO KUTOA UHAI.
Baharia TV
0:00 / 0:00
MAPENZI NI MHIMU ILIA UKIONA MAPENZI HAYAPO CHUKUA HATUA ZA KISHERIA SIO KUTOA UHAI.
102 просмотра · 9 ч назад
Baharia TV
108 тыс. подписчиков
102 просмотра · 9 ч назад
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi (ACP) Gallus Hyera amewataka wananchi wa Dodoma kuepuka kufanya vitendo vya kikatili ambavyo vimekuwa ni kinyume na Sheria na kuleta taharuki katika Jamii.
Hayo yamejiri Oktoba 10, 2026 katika kampeni ya "Ongea na Kamanda" iliyo enda sambamba na zoezi la kufanya usafi katika soko la Chang'ombe ambapo Kamanda Hyera amesema kumekuwa na dhana ya baadhi ya wananchi kujichukulia Sheria mkono na kupoteza uhai wa mtu huku chanzo kikiwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda Hyera amesema kufanya kitendo hicho. Cha kutoa uhai wa mtu chanzo kikiwa ni wivu wa mapenzi au migoro huo ni uhalifu ambao Jeshi la Polisi Litachukua hatua stahiki Kwa kitendo hicho.
#BahariaNews
"Nitoe rai Kwa wanaume, wanawake kuacha vitendo hivyo na pindi inapotekea mgogoro katika familia toeni taarifa Kwa Jeshi la Polisi mapema Kuna dawati pia la Jinsia pamoja na mamla zinasosimamia masuala hayo, msisubiri mpaka itokee athari ndio mripoti" amesema ACP Hyera.
Katika hatua nyengine Kamanda Hyera amewataka wananchi kuwatumia Polisi kata waliopo katika maeneo yao kutoa taarifa za uhalifu pamoja na changamoto nyenginezo za kiusalama.
Wananchi wa kata ya chang'ombe wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa katika kata hiyo ambapo biashara katika soko zimekuwa zikifanyika nyakati za mchana na usiku