MFANYA BIASHARA WA MIFUGO SAILEPU SATULO WA KIJIJI CHA LEPURKO AFANYA MAAMUZI BORA
Mtazame Kristo Tv
0:00 / 0:00
MFANYA BIASHARA WA MIFUGO SAILEPU SATULO WA KIJIJI CHA LEPURKO AFANYA MAAMUZI BORA
2 397 просмотров · 3 недели назад
Mtazame Kristo Tv
91,2 тыс. подписчиков
2 397 просмотров · 3 недели назад
MFANYABIASHARA WA MIFUGO SAILEPU SATULO AGEUZA UTAJIRI WA MIFUGO KUWA NYUMBA YA KISASA LEPURKO, MBUNGE ISACK JOSEPH ATOA PONGEZI
Monduli, Arusha
Mfanyabiashara maarufu wa mifugo kutoka jamii ya Kimaasai, Sailepu Satulo, ameandika historia mpya katika Kijiji cha Lepurko, Wilaya ya Monduli, baada ya kugeuza mafanikio aliyoyapata kupitia biashara ya mifugo na kujenga nyumba ya kisasa inayotajwa kuwa mfano wa maendeleo kwa jamii ya wafugaji.
Uzinduzi wa nyumba hiyo ulifanywa na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe. Isack Joseph Copriano, ambaye alimpongeza Sailepu Satulo kwa kutumia mapato ya mifugo kuwekeza katika makazi bora na kuwa chachu ya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Monduli.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Isack alisema kuwa hatua ya Sailepu inaonyesha wazi kuwa ufugaji unaweza kuwa chanzo kikubwa cha maendeleo endapo utasimamiwa kwa weledi na mapato yake kutumika katika uwekezaji wenye tija.