NETANYAHU -"RUBANI ALIYEMCHOMA KISU MWENZAKE ALIKUSUDIA KUIANGUSHA NDEGE"...
Global TV Online
0:00 / 0:00
NETANYAHU -"RUBANI ALIYEMCHOMA KISU MWENZAKE ALIKUSUDIA KUIANGUSHA NDEGE"...
18 746 просмотров · 17 часов назад
Global TV Online
5,95 млн подписчиков
18 746 просмотров · 17 часов назад
NETANYAHU -"RUBANI ALIYEMCHOMA KISU MWENZAKE ALIKUSUDIA KUIANGUSHA NDEGE"...
@ONESMO - DAR
CC; OTIENO
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema ushahidi wa awali unaonyesha kuwa mmoja wa marubani wa ndege ya Flydubai iliyokuwa ikisafiri kutoka Dubai kuelekea Tel Aviv alikusudia kuangusha ndege hiyo baada ya kumshambulia na kumchoma kisu rubani mwenzake ndani ya chumba cha marubani. Netanyahu amesema tukio hilo lilikuwa tukio kubwa sana la kiusalama na lilitokea wakati ndege hiyo ikiwa njiani kuelekea Israel, ikiwa imewabeba abiria wengi ambao walikuwa raia wa Israel.
Netanyahu amesema kwa mujibu wa taarifa alizopokea, mmoja wa marubani alimshambulia mwenzake na kumchoma kisu, kisha ndege hiyo ikaonekana kuanza kupoteza udhibiti. Amesema abiria mmoja wa Israel aliyekuwa ndani ya ndege alimweleza kuwa ndege ilianza kushuka kwa kasi na kuingia katika hali ya hatari, jambo lililozua hofu kubwa miongoni mwa abiria. Taarifa za ufuatiliaji wa ndege zinaonyesha kuwa ndege hiyo ilishuka kwa kasi kutoka mwinuko wa takribani futi 33,000, huku ikipoteza karibu futi 14,000 kwa muda mfupi kabla ya hali hiyo kudhibitiwa.
============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com