Перейти к содержимому

MAKAMU WA RAIS ASISITIZA TEKNOLOJIA IWE NYENZO MUHIMU UKUSANYAJI WA KODI

MUUNGANO TV

0:00 / 0:00

MAKAMU WA RAIS ASISITIZA TEKNOLOJIA IWE NYENZO MUHIMU UKUSANYAJI WA KODI

91 просмотр · 9 дней назад
MUUNGANO TV
3,5 тыс. подписчиков
91 просмотр · 9 дней назад
MAKAMU WA RAIS ASISITIZA TEKNOLOJIA IWE NYENZO MUHIMU UKUSANYAJI WA KODI, ATOA WITO MKUTANO WA CATA UONGOZE MATOKEO YANAYOPIMIKA YA NDANI NCHI. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema ni muhimu teknolojia kuwa nyenzo muhimu ya kusaidia katika kukusanya mapato ya ndani kwa ufanisi na haki ili nchi ziweze kufadhili shughuli zao na vipaumbele vya maendeleo kupitia rasilimali za ndani. Makamu wa Rais ametoa wito huo, wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Mkutano wa 46 wa Chama cha Wasimamizi wa Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA) unaofanyika katika Ukumbi wa Gran Melia Jijini Arusha. Amesema mfumo mzuri wa kodi unapaswa kuwa wa uhakika, kuwezesha biashara halali, kuhimiza uwekezaji na urasimishaji, na kuwezesha sekta binafsi kutumia nafasi yake ya kuchagiza mabadiliko ya kiuchumi kama ilivyokusudiwa chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania 2050. Ameongeza kwamba ukusanyaji wa kodi usizuie shughuli za kiuchumi zenye tija bali kuunga mkono shughuli hizo.