Перейти к содержимому

Kardinali Rugambwa: Ole wetu kama tutawasahau ndugu zetu waliotangulia mbele za haki.

Breez Online Tv

0:00 / 0:00

Kardinali Rugambwa: Ole wetu kama tutawasahau ndugu zetu waliotangulia mbele za haki.

958 просмотров · 4 дня назад
Breez Online Tv
93,1 тыс. подписчиков
958 просмотров · 4 дня назад
OLE WETU TUKIWASAHAU WALIOTUTANGULIA MBELE ZA HAKI – KARDINALI RUGAMBWA BUKOBA: Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa amewataka waamini kuendelea kuwakumbuka na kuwaombea ndugu na wapendwa wao waliotangulia mbele za haki, akisisitiza kuwa maisha yao yameacha alama ya pekee kwa wale waliowaacha duniani. Kardinali Rugambwa ameyasema hayo katika Misa Takatifu ya Kumuombea Marehemu Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, iliyofanyika katika Jimbo Katoliki la Bukoba. Amesema waliotangulia walikuwa sehemu ya maisha ya walio hai, waliwapa upendo, walijitoa kwa ajili ya wengine na, kwa kufuata mfano wa Yesu Kristo, walifanya mambo yaliyowasaidia wengine kuwa walivyo leo. Kardinali Rugambwa amesisitiza kuwa sababu ya kuendelea kuwakumbuka ni kwa kuwa maisha yao hayakuwa laana bali yalikuwa uhai na baraka, huku kila mmoja akiwa ameacha historia na ushuhuda wake kwa familia, jamii na jumuiya ya Kikristo. Ameonya kuwa kuwasahau waliotutangulia ni kupoteza sehemu ya upendo na historia waliyotuachia, akiwataka waamini kuendelea kuwapenda, kuwakumbuka na kuwaombea, kwa kuwa wameacha alama isiyofutika katika maisha ya walio hai. Imeandikwa na Izahaki Mwacha Video Source: Radio Mbiu #KanisaKatoliki #Tanzania #news #Nairobi #mkombozicommercialbank #BaloziwaAmani #woisooriginalproducts #breezonlinetv