Перейти к содержимому

BODABODA RUKWA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA BARABARANI

CLOUDS HABARI

0:00 / 0:00

BODABODA RUKWA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA BARABARANI

9 просмотров · 1 день назад
CLOUDS HABARI
1,92 тыс. подписчиков
9 просмотров · 1 день назад
BODABODA RUKWA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA BARABARANI Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda mkoani Rukwa wametakiwa kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani, hatua inayolenga kupunguza ajali na kulinda maisha yao pamoja na watumiaji wengine wa barabara. Wito huo umetolewa na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Chapruma Gama, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Rukwa, anayesema usalama wa chombo cha usafiri unaanzia kwa dereva mwenyewe kwa kuzingatia sheria na taratibu za barabarani. Kwa upande wao, wananchi wamewataka madereva hao kuzingatia alama za barabarani na kuwa makini wanapowahudumia abiria, hususan katika maeneo yenye watembea kwa miguu, ili kuepusha ajali zinazoweza kusababisha madhara. Aidha, viongozi na madereva wa bodaboda wamesema vyama vyao vimeweka kanuni zinazowabana wanachama wanaokiuka taratibu, hatua ambayo wameeleza imesaidia kwa kiasi fulani kupunguza vitendo vinavyoweza kusababisha ajali. Wameomba pia kurahisishwa kwa upatikanaji wa leseni za udereva, wakieleza kuwa leseni ni miongoni mwa vigezo vinavyohitajika katika kupata mikopo kutoka baadhi ya taasisi za fedha.