Перейти к содержимому

🔴VURUGU WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU,WATATU WAFA,25 MBARONI

Toka zamani Tv

0:00 / 0:00

🔴VURUGU WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU,WATATU WAFA,25 MBARONI

359 просмотров · 7 часов назад
Toka zamani Tv
155 тыс. подписчиков
359 просмотров · 7 часов назад
VURUGU WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU,WATATU WAFA,25 MBARONI Watu watatu wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika mfululizo wa matukio yanayodaiwa kuchochewa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji wilayani Tunduru, huku Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma likiwakamata watu 25 wanaodaiwa kuhusika na mauaji na vurugu hizo. Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya, baada ya kufika katika maeneo yaliyoathiriwa na kujionea uharibifu wa mali uliotokana na vurugu hizo, ikiwemo kuchomwa kwa ofisi za Serikali na kuharibiwa kwa gari la Polisi. Kwa mujibu wa Kamanda Chilya, kati ya watuhumiwa 25 waliokamatwa, wanane wanahusishwa na matukio ya mauaji huku 17 wakihusishwa na vurugu, ambapo wafugaji ni 10 na wakulima 15. Ameongeza kuwa operesheni na upelelezi vinaendelea ili kuwabaini na kuwakamata wahusika wengine. Mfululizo wa matukio hayo ulianza Septemba 17, 2026, katika Kijiji cha Mrusha, Tarafa ya Lukumbule, baada ya mfugaji Shimbi Upole Shimbi, mwenye umri wa miaka 45, kutoa taarifa kuwa ng’ombe wake 180 waliporwa na kundi la wananchi wanaodaiwa kuwa wakulima na kuondoka nao kuelekea Kijiji cha Chikomo. Taarifa hiyo inaeleza kuwa mfugaji huyo, akiwa na ndugu zake, alianza kuwatafuta ng’ombe hao na kufanikiwa kuwapata 179 katika pori la Kijiji cha Chinunje, Kata ya Mbesa, Tarafa ya Nalasi, huku ng’ombe mmoja pamoja na mchungaji Msanja Shimbi Upole wakiwa hawajaonekana. Septemba 18, 2026, wafugaji walimtafuta mchungaji huyo na kumkuta ameuawa, mwili wake ukiwa umezamishwa kwenye matope katika Mto Chermambo, Kijiji cha Chinunje. Baada ya tukio hilo, wafugaji walivamia Vijiji vya Chikomo na Chinunje, ambapo Mohamed Kasim Chabwela, mwenye umri wa miaka 58, aliuawa, huku watu wawili, Yusuph Yasin Bakili, mwenye umri wa miaka 42, na Rashid Ally Ahmad, mwenye umri wa miaka 49, wakijeruhiwa. SUBSCRIBE HERE:www.youtube.com/c/tokazamanitv?sub_co...