BIN LADEN: FAMILIA ILIYOJENGA SAUDI ARABIA - MTOTO AKAGEUKA ADUI WA DUNIA
Simulizi Zinaishi
0:00 / 0:00
BIN LADEN: FAMILIA ILIYOJENGA SAUDI ARABIA - MTOTO AKAGEUKA ADUI WA DUNIA
20 899 просмотров · 5 дней назад
Simulizi Zinaishi
34,4 тыс. подписчиков
20 899 просмотров · 5 дней назад
Kabla jina Osama bin Laden halijawa moja ya majina yaliyotafutwa zaidi duniani, kulikuwa na hadithi nyingine, hadithi ya familia.
Kutoka Hadhramaut, Yemen, Mohammed bin Laden aliwasili Saudi Arabia akiwa mhamiaji mwenye maisha ya kawaida. Miaka iliyofuata, alijenga kampuni kubwa ya ujenzi na familia yake ikawa sehemu muhimu ya historia ya maendeleo ya Saudi Arabia.
Ndani ya familia hiyo alizaliwa Osama bin Laden.
Alikulia katika utajiri, akasoma, akakutana na mazingira ya kidini na kisiasa yaliyokuwa yakibadilika katika ulimwengu wa Kiislamu, mpaka vita vya Afghanistan vikampeleka kwenye njia ambayo ingebadilisha maisha yake, na baadaye kubadilisha historia ya dunia.
Lakini safari haikuishia Afghanistan.
Osama alirudi Saudi Arabia, akagongana na serikali yake kuhusu uwepo wa wanajeshi wa Marekani katika ardhi ya Saudi Arabia, akapoteza uraia wake na mali zake zikadhibitiwa.
Kisha akaenda Sudan.
Huko akajenga maisha mapya ya biashara na mitandao, kabla ya shinikizo la kimataifa kumlazimisha kuondoka tena.
Hatimaye akarudi Afghanistan.
Mnamo 1996, alitoa tamko lake maarufu dhidi ya wanajeshi wa Marekani waliokuwa Saudi Arabia akilitaja eneo hilo kama “Land of the Two Holy Places.”
Hii si documentary ya kurudia 9/11, mashambulizi ya Afrika Mashariki au Operation Neptune Spear kwa undani. Matukio hayo tayari tumeyasimulia katika documentaries nyingine.
Safari hii tunarudi nyuma zaidi:
Osama alikuwa nani kabla hajawa Osama bin Laden ambaye dunia ilimjua?
Familia yake ilitoka wapi?
Baba yake alijengaje himaya?
Ni mazingira gani yaliyomlea?
Na ni kwa nini mtoto wa familia iliyokuwa karibu na mfumo wa Saudi Arabia alifika mahali pa kuugeukia mfumo huo?
Na baada ya Osama…
nani alibeba kivuli chake?
Safari hii itaendelea katika simulizi la Hamza bin Laden, mwana aliyebeba jina, historia na urithi wa Osama.
Karibu kwenye historia.
SIZ Media — Simulizi Zinaishi.