SOMO: NAMNA YA KUPIGANA NA PEPO ALIYEPITIA MLANGO WA MANENO (4)
Mch. Raphael Joshua
0:00 / 0:00
SOMO: NAMNA YA KUPIGANA NA PEPO ALIYEPITIA MLANGO WA MANENO (4)
1 747 просмотров · 3 г. назад
Mch. Raphael Joshua
7,51 тыс. подписчиков
1 747 просмотров · 3 г. назад
SOMO: NAMNA YA KUPIGANA NA PEPO ALIYEPITIA MLANGO WA MANENO
MHUBIRI: MCH. RAPHAEL JOSHUA
KLPT – KILUVYA KWA KOMBA
Sehemu ya 4
Watu wengi katika jamii wanapitia mateso makali kutokana na maneno yaliyotamkwa na watu waliokufa.
Watu waliokufa anaweza kuwa baba/mama/babu/bibi au mchawi ama mganga au mtu yeyote ambaye alitamka maneno fulani ambayo nyuma yake kuna nguvu ya roho chafu. Maneno hayo yalitamkwa na mtu huyo kwa sababu mbalimbali inaweza kuwa wivu, hasira, uchungu au husuda juu ya mtu fulani wakati wa uhai wake. Yanaweza kuwa yalitamkwa kwa siri ama hadharani na kwa sababu nyuma yake yana nguvu ya roho chafu yakaishi na kutengeneza mfumo wa utekelezaji wake katika maisha ya walio hai.
Baada ya mtu aliyeyatamka kufa, maneno yake hayakufa kwa sababu nyuma yake yalikuwa na roho fulani ambayo inatenda kazi hata baada ya kufa aliyetamka hayo maneno.
Maneno ya laana ya wafu yanaweza kutengeneza mfumo wa magonjwa, umaskini, utasa, kutokuoa au kuolewa au ukuta unaozuia mafanikio ya mtu katika maisha yake.
Ili kujinasua kutoka kwenye nguvu ya maneno ya wafu unahitaji kuwa na ufahamu na maarifa ya kutosha kufuta na kupigana na pepo wanaomtesa mtu kutokana na nguvu ya hayo maneno.
Somo hili linakufundisha namna ya kushughulika na kushinda NGUVU YA MANENO YA WAFU INAYOATHIRI MAISHA YA WATU WALIO HAI.
FUATILIA SOMO HILI KWA KINA