Darsa: الصدمات النفسية 🔴LIVE DARSA| TRAUMA (Kihoro) na AFYA ya AKILI (II)
Darsa na Mihadhara
0:00 / 0:00
Darsa: الصدمات النفسية 🔴LIVE DARSA| TRAUMA (Kihoro) na AFYA ya AKILI (II)
173 просмотра · 1 мес. назад
Darsa na Mihadhara
886 подписчиков
173 просмотра · 1 мес. назад
Darsa ilifanyika Rabi'uth Thani 09, 1447H Jumapili Septemba 20, 2026
SEHEMU YA PILI
الصدمات النفسية
كيف تؤثر الصدمة النفسية في الجسد، العقل، النَّفْس، القلب، و الإيمان؟ من منظور علم النفس الإسلامي
TRAUMA (Kihoro) na afya ya akili (Mental Health)
Jinsi kihoro kinavyoathiri mwili, akili, nafsi, moyo na imani
Trauma/kihoro/kiwewe:
KWANZA: Maana yake ni: Huzuni kubwa inayoweza kupatikana kutokana na kufikwa na jambo la msiba.
Kihoro/kiwewe cha kisaikolojia au kiwewe cha kihisia ni mwitikio wa kihisia unaotokea baada ya mtu kufikiwa au kupatwa na tukio la kushtua au la kuogofya, au kupitia uzoefu wenye uchungu unaoambatana na madhara ya kisaikolojia na pengine kimwili.
PILI: Malengo ya kujifunza Kihoro
TATU: Sababu za kujifunza kihoro
NNE: Aina za kihoro/majeraha ya kisaikolojia:
1. Kihoro/kiwewe cha papo kwa hapo: Kihoro cha papo kwa hapo kinafafanuliwa kama ni mwitikio wa kihisia unaotokana na kufikwa au kupatwa na tukio mahususi la kihoro.
2. Kihoro cha kudumu ni: Mwitikio wa kihisia wa muda mrefu unaotokana na mfiduo unaorudiwa na unaoendelea kwa matukio hatari na ya mkazo kwa miezi au miaka. Kama vile unyanyasaji wa watoto, uonevu, au unyanyasaji wa majumbani.
3.Kihoro kigumu ni: Hali ya kihoro cha kisaikolojia ambayo hutokea kutokana na kufikwa na mfululizo wa matukio au hali zenye uchungu na kuacha athari ya kudumu kwenye nafsi.
TANO: Athari zake
SITA: Tiba/Matibabu yake
SABA: Mtazamo wa Kiislamu na wa kisaikolojiakuhusiana na kihoro/kiwewe.