WAFANYABIASHARA WA NYAMA ISIOLO WATAKA USALAMA KUIMARISHWA BARABARA YA KUELEKEA KICHINJIO KIKUU
𝐖𝐀𝐒𝐎 𝐓𝐕
0:00 / 0:00
WAFANYABIASHARA WA NYAMA ISIOLO WATAKA USALAMA KUIMARISHWA BARABARA YA KUELEKEA KICHINJIO KIKUU
234 просмотра · 5 дн. назад
𝐖𝐀𝐒𝐎 𝐓𝐕
7,31 тыс. подписчиков
234 просмотра · 5 дн. назад
Wafanyabiashara wa bucha katika mji wa Isiolo wametoa wito wa kuimarishwa kwa usalama katika barabara inayoelekea kwenye Kichinjio Kikuu cha Kisasa cha Isiolo, kufuatia kubomolewa kwa kichinjio cha zamani.
Wafanyabiashara hao wamesema kuwa kuimarishwa kwa usalama katika barabara hiyo ni muhimu ili kuhakikisha wanasafirisha mifugo yao hadi kichinjioni kwa ajili ya kuchinjwa bila kuhatarisha maisha yao na mali zao.
Aidha, wametoa wito kwa Rais William Ruto na Gavana wa Isiolo, Abdi Ibrahim Hassan Guyo, kuchukua hatua za kuhakikisha usalama unaimarishwa katika eneo hilo ili kuwawezesha kuendesha shughuli zao za biashara bila hofu.
Wamesisitiza kuwa hatua madhubuti za kiusalama zinahitajika ili kulinda wafanyabiashara na kuhakikisha kuwa shughuli za biashara ya nyama zinaendelea bila vitisho au vikwazo.
Join this channel to get access to perks:
/ @wasotv
WASO TV - Informing and Entertaining