IRAN YAONYA TRUMP ASIWAPOTOSHE - HAKUNA MAZUNGUMZO YOYOTE - YATAKA MASHARTI YATIMIZWE
Global TV Online
0:00 / 0:00
IRAN YAONYA TRUMP ASIWAPOTOSHE - HAKUNA MAZUNGUMZO YOYOTE - YATAKA MASHARTI YATIMIZWE
5 992 просмотра · 11 часов назад
Global TV Online
5,94 млн подписчиков
5 992 просмотра · 11 часов назад
IRAN YAONYA TRUMP ASIWAPOTOSHE - HAKUNA MAZUNGUMZO YOYOTE - YATAKA MASHARTI YATIMIZWE
@ONESMO - DAR
CC; OTIENO
Iran imekataa uwezekano wa kuanza tena mazungumzo na Marekani kuhusu vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati, licha ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema kuwa Washington iko tayari kuangalia uwezekano wa kurejea kwenye mazungumzo na Tehran. Msimamo huo umetolewa na Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, baada ya Trump kutoa kauli inayodokeza kuwa Marekani inaweza kushiriki mazungumzo mapya na Iran.
Rezaei alitoa msimamo huo kupitia mtandao wa X, akiwataka Wairani wasipotoshwe na kile alichokiita ujumbe unaokinzana kutoka kwa Rais Trump. Katika ujumbe wake, Rezaei aliandika: “Usiruhusu ishara mchanganyiko kutoka kwa rais wa Marekani zikukengeushe — kutoka ‘hakuna mazungumzo’ hadi ‘tuko tayari kuzungumza.’” Kauli hiyo imekuja wakati ambapo Trump amebadilisha kwa kiasi fulani msimamo wake wa awali kuhusu uwezekano wa kufanya makubaliano na Iran.
============================================================
⚫️ JE, UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 760 403894 or 255 719 401968)
⚫️ Email: globaltvonline.newsdesk@gmail.com