Перейти к содержимому

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA FRIDAY PRAYERS 16 OCTOBER 2026

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH

0:00 / 0:00

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA FRIDAY PRAYERS 16 OCTOBER 2026

8 590 просмотров · Трансляция закончилась 6 часов назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
65,6 тыс. подписчиков
8 590 просмотров · Трансляция закончилась 6 часов назад
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA FRIDAY PRAYERS 16 OCTOBER 2026 UJUMBE WA LEO : JIWE LA DAUDI KWENYE MKONO WAKO ( VAZI LA NGUVU ZAKO ) NENO KUU : 1 SAMWELI 17 : 48 - 50 48 Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti. 49 Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi. 50 Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake. AGENDA ZA MAOMBI KATIKA MLIMA WA MAOMBI IJUMAA 1. Omba kusimama kinyume na vikao vya wazi na vya siri vya uharibifu juu ya kile Mungu ameweka kwenye mikono yako. Mwanzo 37 : 18 18 Wakamwona toka mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue. 2. Omba kuvua vazi la uharibifu katika Ulimwengu wa Roho Zaburi 109 : 29 29 Washitaki wangu watavikwa fedheha, Watajivika aibu yao kama joho. Isaya 42 : 22 22 Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha. 4. Omba Mungu akuondolee Roho nzito na usingizi Roho ya kupuuzia Roho Mtakatifu Isaya 29 : 10 10 Kwa maana Bwana amewamwagieni roho ya usingizi, amefumba macho yenu, yaani, manabii; amefunika vichwa vyenu, yaani, waonaji. 5. Ombea njia yako Duniani Mwanzo 6 : 12 12 Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani. Mhubiri: Mwl.Mwinjilisti Henry mlay Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com