Перейти к содержимому

TAIKO OLE KULUNJU AIPONGEZA SERIKALI KUSOGEZA UMEME VIJIJINI SIMANJIRO

OLDONYO MEDIA

0:00 / 0:00

TAIKO OLE KULUNJU AIPONGEZA SERIKALI KUSOGEZA UMEME VIJIJINI SIMANJIRO

1 615 просмотров · 5 дней назад
OLDONYO MEDIA
10,5 тыс. подписчиков
1 615 просмотров · 5 дней назад
TAIKO OLE KULUNJU AIPONGEZA SERIKALI KUSOGEZA UMEME SIMANJIRO Mdau wa maendeleo wilayani Simanjiro, Taiko Ole Kulunju, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusogeza huduma ya umeme hadi vijijini, akisema huduma hiyo imefika katika maeneo ambayo awali ilikuwa vigumu kutarajia kuifikia. Kulunju ameyasema hayo katika sherehe ya Ntimayo Kiambwa iliyofanyika Terrati, ambapo amempongeza kwa kuendeleza mila na desturi za jamii kupitia Jando, akisema kuwaalika wanajamii kushiriki ni ishara ya umoja na mshikamano. Diwani wa Kata ya Terrati, Jackson Materi, amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo, akisisitiza umuhimu wa kuweka pembeni siasa na kuelekeza nguvu katika shughuli za maendeleo. Naye Mwenyekiti wa CCM Kata ya Terrati, Ole Koromo, amempongeza Kulunju kwa mchango wake katika shughuli mbalimbali za maendeleo ndani na nje ya Simanjiro, akisema juhudi zake zimeendelea kuwa na manufaa kwa jamii.