Перейти к содержимому

🛑LIVE: UCHEBE YANGA AMPASUA PRISCA YANGA/ AMETUKOSEA SANA/ KWANI ALIAMBIWA UWANJA HAUTAJENGWA?

Prosper Tv

0:00 / 0:00

🛑LIVE: UCHEBE YANGA AMPASUA PRISCA YANGA/ AMETUKOSEA SANA/ KWANI ALIAMBIWA UWANJA HAUTAJENGWA?

961 просмотр · 4 месяца назад
Prosper Tv
8,72 тыс. подписчиков
961 просмотр · 4 месяца назад
Shabiki na mwanachama wa Young Africans SC, anayefahamika kwa jina la Uchebe Yanga, ametoa maoni yake kufuatia kitendo cha mwanachama mwenzake Prisca Yanga kwenda katika makao makuu ya klabu hiyo na kurekodi eneo hilo, huku akitoa madai kuwa mradi wa ujenzi wa uwanja katika eneo hilo haujaanza kutekelezwa kama ilivyoahidiwa na uongozi wa klabu. Prisca alionekana katika eneo hilo akirekodi video na kuhoji hatua ya utekelezaji wa ahadi ya uwanja, jambo lililoibua mjadala miongoni mwa wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuhusu uwazi wa miradi ya maendeleo ndani ya Yanga. Hata hivyo, Uchebe amekosoa vikali kitendo hicho, akisema kilipaswa kufanyika kwa njia sahihi na kwa kuzingatia taratibu za klabu badala ya kuchukua hatua binafsi na kuingia katika eneo hilo bila ridhaa ya viongozi. Amesema kuwa masuala ya maendeleo ya klabu yanahitaji ufuatiliaji wa kina na taarifa sahihi kutoka kwa uongozi, badala ya kufanya matukio ya kujitegemea ambayo yanaweza kuchochea sintofahamu miongoni mwa wanachama na mashabiki.