WAKAZI WA LMD WAFUNGA BARABARA KUPINGA MAUAJI
𝐖𝐀𝐒𝐎 𝐓𝐕
0:00 / 0:00
WAKAZI WA LMD WAFUNGA BARABARA KUPINGA MAUAJI
214 просмотров · 8 часов назад
𝐖𝐀𝐒𝐎 𝐓𝐕
7,2 тыс. подписчиков
214 просмотров · 8 часов назад
Wakazi wa LMD, katika Wadi ya Burat, Kaunti ya Isiolo, wamefunga barabara inayounganisha Kipsing na Oldonyiro, wakipinga mauaji ya mvulana mwenye umri wa miaka 15.
Mvulana huyo alipigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa wahalifu alipokuwa akichanja kuni, na kuaga dunia papo hapo.
Wakazi hao walifunga barabara hiyo kwa mawe na matawi ya miti, wakionyesha ghadhabu kufuatia mauaji hayo. Maafisa wa polisi walifika katika eneo hilo na kutuliza hali.
Akizungumza na wanahabari, Mwakilishi wa Wadi ya Burat, Nicholas Lorot, ameitaka Serikali ya Kitaifa kuongeza idadi ya maafisa wa usalama katika eneo hilo ili kuimarisha doria na kukabiliana na wahalifu ambao, kwa mujibu wake, wamekuwa wakiwashambulia na kuwaua wakazi.
Lorot pia amedai kuwa zoezi la unyang’anyi wa bunduki lililofanyika katika eneo hilo liliwalenga wanajamii wa jamii moja pekee. Ameitaka serikali kuhakikisha zoezi hilo linafanywa kwa usawa na bila ubaguzi.
Kwa upande wake, Gabriel Lekutan, ambaye ni msaidizi wa Mbunge wa Isiolo Kaskazini, Joseph Samal, amekashifu mauaji ya mvulana huyo na kuitaka serikali kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha usalama wa wakazi.
Lekutan amesema serikali inapaswa kuwajibika ipasavyo na kuwachukulia hatua wahalifu ambao, kwa mujibu wake, wamekuwa wakihusika na mauaji ya mara kwa mara katika eneo hilo.
Wakati huo huo, Augustine Eregae, mgombeaji wa kiti cha uwakilishi wa Wadi ya Burat, amemtaka Waziri wa Usalama wa Kitaifa, Kipchumba Murkomen, kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha usalama wa wananchi unalindwa.
Eregae ameonya kuwa iwapo serikali haitachukua hatua za haraka kukabiliana na uhalifu katika eneo hilo, wakazi wanaweza kuamua kuchukua hatua za kujilinda wenyewe dhidi ya wahalifu ambao, kwa mujibu wake, wamekuwa wakiwahangaisha kwa muda.
Join this channel to get access to perks:
/ @wasotv
WASO TV - Informing and Entertaining