Перейти к содержимому

RAIS HAAMBIWI UKWELI - MOHAMMED ALI

ZANZIBAR YETU

0:00 / 0:00

RAIS HAAMBIWI UKWELI - MOHAMMED ALI

395 просмотров · 3 дня назад
ZANZIBAR YETU
10,8 тыс. подписчиков
395 просмотров · 3 дня назад
Mwakilishi wa Wananchi Jimbo la Ziwani, Mohammed Ali Salum, alisema ana imani kuwa Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi atasikiliza kilio cha wananchi hao na kusaidia kupatikana kwa ufumbuzi. Alisisitiza umuhimu wa kuzingatia hali za wananchi wenye kipato cha chini ambao wamewekeza fedha zao katika ujenzi wa nyumba za kuishi. Awali Wananchi wa Kijiji cha Kwarara, Wilaya ya Magharibi B, Unguja, wameiomba Serikali ya Zanzibar (SMZ) kupitia Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), kupima na kuweka wazi eneo linalohitajika kwa ajili ya hifadhi ya huduma ya maji safi ili kuwawezesha wananchi kujua hatima ya maeneo yao na ujenzi wa nyumba zao. Ombi hilo limetolewa leo mbele ya timu ya Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi kupitia ACT Wazalendo, Prof. Omar Fakih Hamad, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kusikiliza changamoto na kero zinazowakabili wananchi wa Zanzibar. Haruna Haji Ame, Mwenyekiti wa CCM wa Tawi la Kwarara, aliiomba ZAWA kupima mita 50 zinazohitajika kwa ajili ya hifadhi ya maji na kuwaachia wananchi eneo litakalobaki waendelee na ujenzi wa nyumba zao. Kwa upande wake, Othman Ali Othman alisema wananchi wamekuwa katika hali ya sintofahamu kutokana na madai ya kupimiwa maeneo tofauti mara kwa mara. Aliiomba Serikali kuingilia kati na, iwapo eneo hilo linahitajika kwa huduma ya maji, iwatafutie wananchi maeneo mbadala. Naye Salama Khamis Mbarouk aliiomba Serikali kuwaachia eneo hilo au kuwapatia fidia itakayowawezesha kununua maeneo mengine ya kujenga. Akizungumza kwa hisia, Fatma Juma Muhammed alimuomba Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuwahurumia wananchi ambao tayari wameanza ujenzi lakini hawana uwezo wa kuhamia maeneo mengine. “Mimi ni mwanamke, nakuomba Rais wangu Dk. Mwinyi uniangalie kwa hali nyingine. Mimi sina uwezo wa kuliondoa tofali na sina pa kupeleka,” alisema Fatma. Alidai kuwa wananchi walizuiwa kuendelea na ujenzi bila kupewa barua rasmi za zuio, licha ya baadhi yao kupewa barua za kuomba vibali vya ujenzi na viongozi wa Serikali ya Shehia. “Masheha wametupatia barua za kuomba vibali vya ujenzi, lakini ZAWA wanatuletea askari wakidai haturuhusiwi kujenga,” alisema Fatma. Wananchi wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kwa kuweka wazi mipaka ya eneo la hifadhi ya maji na kutafuta suluhisho litakalolinda mahitaji ya huduma ya maji safi huku likizingatia hali za wananchi walioanza ujenzi wa nyumba zao. Seif Haji Shehe, mkazi wa eneo hilo, alisema tayari amejikusanya kwa muda mrefu na kufanikiwa kujenga nyumba yake kwa uwezo wake, hivyo kusimamishwa kwa ujenzi kumemweka katika hali ngumu.